Mchezaji staa wa Real Madrid
Cristiano Ronaldo ameweka wazi kwamba anatamani aendelee kuichezea club
hiyo kwenye maisha yake yote ya soka yaliyobaki.
Gazeti ya Uingereza (The Sun) limeandika kwamba Ronaldo amesema kama ingekua ni uwezo wake angesaini hata mkataba wa miaka kumi wa kuichezea club hiyo ila hilo linashindikana kwa sababu kuna taratibu zilizowekwa na club.
Ronaldo ambae anajiandaa na Euro 2012 mpaka sasa ameshaifungia Real Madrid magoli 112 toka ajiunge nayo mwaka 2009 ambapo inakua club ya kwanza yeye kuifungia magoli mengi toka aanze soka, aliifungia Manchester United magoli 84 wakati alipoichezea kuanzia 2003-2009.
Gazeti ya Uingereza (The Sun) limeandika kwamba Ronaldo amesema kama ingekua ni uwezo wake angesaini hata mkataba wa miaka kumi wa kuichezea club hiyo ila hilo linashindikana kwa sababu kuna taratibu zilizowekwa na club.
Ronaldo ambae anajiandaa na Euro 2012 mpaka sasa ameshaifungia Real Madrid magoli 112 toka ajiunge nayo mwaka 2009 ambapo inakua club ya kwanza yeye kuifungia magoli mengi toka aanze soka, aliifungia Manchester United magoli 84 wakati alipoichezea kuanzia 2003-2009.
KAZI POPOTE

.
Baada ya mtangazaji wa kituo
cha radio cha Hot 97 New York Marekani Peter Rosenberg kupanda kwenye
stage ya tamasha kubwa la Summer Jam na kutoa maneno ambayo yalionekana
kumlenga Nicki Minaj kwa hiphop ya biashara anayoifanya, Nick Minaj
ameamplfy sababu zilizomfanya agome kupanda kwenye stage kuperform baada
ya kusikia hiyo kauli.Nicki amesema hayo maneno yalionekana wazi kabisa kumvunjia heshima kwa sababu mtangazaji huyo pamoja na kumponda Nicki alitaja kabisa na jina la wimbo wa Nicki wa Starships ambapo alisema tuko hapa kwa ajili ya real hiphop, yani hiphop ya ukweli kwa hiyo kama umekuja hapa kusikiliza nyimbo kama starships hatuko hapa kwa ajili yako na anaefanya hiphop isiyo real siongei nae.
Baada ya hiyo statement Lil wyne ambae ni boss wa Nicki Minaj alimkataza Nicki kupanda kwenye stage kwa sababu ilikua ni statement ya kuivunjia heshima YMCMB, na baadae Nicki akasema hakuna atakaeivunjia heshima YMCMB Young Money Cash Money.
Lil Wyne alipomkataza Nicki kupanda kwenye stage, aliwakataza na wasanii wengine wote wa YMCMB na wasanii wengine ambao wangepanda nao kwenye stage wakagoma japo sio YMCB.
Kwenye interview ya leo, Nicki Minaj amesema hata kama angeperform asingeperform single ya Starships kwa sababu hiyo consert ya hot 97 ilikua ya hiphop, kwenye usiku huo alikua apande kwenye stage na Beenie Man, Foxy Brown na Cam’ron.
Nicki Minaj amesema anaelewa kwamba inawezekana Peter alikua anatania lakini ikachukuliwa kama ni diss, ila alipaswa kuomba msamaha au kurekebisha lakini hakufanya hivyo, pamoja na hayo Nicki amekiri kwamba atafanya show ya bure kwa watu wake wa New York ambao hawakumuona kwenye consert ya Summer Jam.
Wengine wa Cash Money ambao walitakiwa kuperform kwenye hiyo show lakini hawakuperform japo walikua backstage ni pamoja na Busta na Dj Khaled.……….. hizo hapo chini ni Tweets zilizoandikwa baada ya mtangazaji huyo wa hot 97 kumdiss Nicki Minaj.
Wanamuziki walaani Manny Pacquiao kunyimwa ushindi dhidi ya Tim Bladley
Kama ulikuwa hujui ni
mchezo gani unaopendwa duniani baada ya soka leo jibu utalipata.
Boxing inapendwa jamani!
Alfajiri hii nchini Marekani kulikuwa na pambano la ngumi kati ya Manny Pacquiao
wa Ufilipino na Tim Bladley wa Marekani.
Bladley amepewa ushindi wa
pointi.
Pacquiao, ambaye mwaka huu
umaarufu wake uligeuka kama dini yenye wafuasi wengi ameshinda mapambano saba
mfululizo na imeonekana wazi kuwa ametawala pambano la leo, lakini ameshindwa.
Ameen ya MwanaFA ni sample ya wimbo wa Cecile-Hey
Solothang ndiye aliyeligundua hili na sisi tukaamua kuhakikisha na kukuta kweli Ameen ya MwanaFA ni sample ya wimbo wa Cecile uitwao Hey aliomshirikisha Agent Sasco. Wimbo huu upo kwenye albam yake ya mwaka jana iitwayo Jamaicanization.
Producer wa wimbo huu ambaye ni Dully Sykes amesample wimbo huo kila kitu. Chorus yake mwenyewe Dully ni copy and paste ya chorus ya Cecile. Kipya kwenye Ameen iliyosifiwa sana wiki hii kwa maneno ya maana ya MwanaFA, ni mashairi tu.
Siku zote sampling pamoja na kuwa si jambo baya kihivyo huleta maana mbaya hasa kwa producer ambaye huonekana hana idea kiasi cha kuchukua za wengine.
Sikiliza mwenyewe na useme kama Dully Sykes ameonewa!
Mwaka huu pia Producer Samtimber wa Arusha alijikuta kwenye scandal hii baada ya kucopy na kupaste beat ya G-Unit kutengeneza ngoma ya Lord Eyes na Fid Q 'Neno
'
Watu wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila umri wa miaka 30
(mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume) waliotambulika kuwa ni wachawi mara
baada ya kubanwa na kujitambulisha wamekamatwa majira ya saa 12 asubuhi
leo katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza
wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani
Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa
kwaajili ya sadaka. picha zaidi tembelea www.gsengo.blogspot.com
ARSENAL WAKOMARIA UEFA

Manchester England
“NAONDOKA Arsenal kwenda Manchester City, siyo kwamba naichukia Arsenal, hapana, naipenda sana lakini nakwenda City kufuata makombe.”
Hiyo ni kauli ya kiungo wa Manchester City, Samir Nasri wakati anaondoka kwenye kikosi cha Arsenal na kujiunga na City.
Mshambuliaji huyo jana ndiyo alikuwa chachu ya Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya QPR na kumaliza ukame wa miaka 44 bila kutwaa ubingwa wa England.
Wakati City ikipata bao la tatu, mechi kati ya Manchester United ilikuwa imeshamalizika kwa United kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland, shukrani kwa bao safi lililofungwa na Wayne Rooney.
Lakini haikuwa hivyo, burudani ya kutosha ilikuwa kwenye Uwanja wa Etihad ambao mpaka dakika ya tisini ya mchezo, City ilikuwa nyuma kwa mabao 2-1.
Pablo Zabaleta aliifungia Man City bao la kwanza katika dakika ya 39, Djibril Cisse aliisawazishia timu yake katika dakika ya 48, Jamie Mackie akatupia la pili katika dakika ya 66.
Kiungo wa QPR, Joel Barton, alipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko, Carlos Tevez na kuanzia hapo QPR walilinda lango lao kwa asilimia 90, hali iliyowafanya wawe majaribuni mara kwa mara.
Pamoja na City kushambulia kwa nguvu zote, iliwabidi kusubiri hadi dakika ya tisini ili kupata bao la kusawazisha lililowekwa kimiani na Edin Dzeko lakini ziliongezwa dakika tano na katika dakika ya nne, Sergio Aguero akaifungia timu yake bao la tatu na la ushindi.
Nafasi ya tatu
Arsenal ilipambana na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mchezo mgumu dhidi ya West Bromwich.
Arsenal ilianza kufunga kupitia kwa Yossi Benayoun, Bromwich wakasawazisha kupitia kwa Shane Long katika dakika ya 11, Graeme Dorrans aliifungia timu yake bao la pili katika dakika ya 15.
Lakini Arsenal ilicharuka na kupata mabao mawili kupitia kwa mabeki André Santos katika dakika ya 30 na Laurent Koscielny dakika ya 55.
Tottenham Hortspur, ilimaliza katika nafasi ya nne baada ya kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Fulham, shukrani kwa mabao yaliyofungwa na Emmanuel Adebayor na Jermaine Defoe.
Newcastle imemaliza katika nafasi ya tano baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Everton.
Zilizoshuka
Bolton, Blackburn na Wolves zimeshuka daraja, Bolton ilikubali sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stoke City na kuungana na Blackburn na Wolves ambazo zilishashuka.
Matokeo mengine
Chelsea iliichapa Blackburn mabao 2-1, Norwich ikaichapa Aston Villa 2-1, S
No comments:
Post a Comment