Wednesday, June 13, 2012

Wanamuziki walaani Manny Pacquiao kunyimwa ushindi dhidi ya Tim Bladley



Kama ulikuwa hujui ni mchezo gani unaopendwa duniani baada ya soka leo jibu utalipata.

Boxing inapendwa jamani! Alfajiri hii nchini Marekani kulikuwa na pambano la ngumi kati ya Manny Pacquiao wa Ufilipino na Tim Bladley wa Marekani.

Bladley amepewa ushindi wa pointi.

Pacquiao, ambaye mwaka huu umaarufu wake uligeuka kama dini yenye wafuasi wengi ameshinda mapambano saba mfululizo na imeonekana wazi kuwa ametawala pambano la leo, lakini ameshindwa.

Ndio maana wapenzi wa ngumi duniani wamechukizwa sana na uamuzi huo wa wazi wa kumbeba Bladley. Wengine wanahisi uamuzi huo umepangwa makusudi kwa maslahi ya biashara ili mabondia hao warudiane mwezi November.

No comments:

Post a Comment