Uchambuzi: Piga simu ya Diva, Ray C mtupu!!!
Ule wimbo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu pengine kuliko nyimbo zote mwaka huu wa mtangazaji wa Clouds FM, Loveness aka Diva umeachiwa rasmi jana kwenye internet.Leo unatambulishwa rasmi redioni.
Waliokuwa na muda usiku na access ya internet walihaha kuudownload na kusikiliza Je! Yaliyomo yamo kweli?
Sisi tumeudownload saa kumi na kitu alfajiri na kuusikiliza kwa makini.
Wimbo unaanza kwa sauti ya kimahaba ya Diva iliyoshushwa kidogo kupisha maneno ya producer Lamar ambaye kama kawaida ya nyimbo zake huongea mwanzoni ‘This is the talk of the town blah blah blah’ bila kusahau ‘Exclusive music.’
Diva anaanza kwa chorus yenye maneno ‘nataka kupiga simu kwako wewe wangu baby’ jambo la kwanza linaloweza kukuingia akilini ni ‘Ray C. Yeah, bila kusikiliza sana sauti ya Diva inafanana sana na ya Rehema Chalamila kwenye wimbo huu. Swaggajacking? That’s something she needs to explain by the way!!
Anaendela kusikika akisema ‘Pokea simu yangu honey popote ulipo wangu baby’. Lakini baada ya maneno hayo Diva anaamua kudhihirisha kuwa ni kweli Ray C ni role model wake kwa kuyarudia maneno ya wimbo wa zamani wa Ray C ‘Uko wapi’ yasemamayo “Uko wapi nikufuate niambie nikuache, angalau nikuone japo sauti nisikie.”
Diamond anaingia kwenye verse ya pili akisikikia, “ Ninapowazaga kamchezo kabaya moyo unanizizima” na kupokelewa na sauti ya kitandani ya Diva (we knew it) oooooohh!! Na Diamond analiokoa jahazi la wimbo huu mfupi kwa kuangusha some good melodies!
So sisi tumeionaje ngoma!!! 50-50! Not bad, not so good! Lakini kwa umaarufu wake na wa Diamond chances are itakuwa hit! And by the way siku hizi you don’t need a good song to make a hit, you need fame, money and promotion to make a hit!
Diva anasemaje? “For 2 f--ng hrs zaidi ya watu elf10,500 wame download 'piga simu ... Happiest :-) thanku.” Really? Congrats then.
“Kinachouzaga ni melody. Si zaidi .... U know what I mean. Enjoy piga simu. Thanks 4ya support mlioonyesha usiku huu,” aliongeza Diva.
Followers wake kwenye twitter wanasemaje? Oooh! Ni rahisi kubashiri…. Lmao. Sifaaaaaa!
“OMG! This song is off the hook.....hiyo Sauti Sasa*Am speechless,aiseee* Nice work bibie..... @Divaakamimi *Kissesss!”
“Piga cm is such a nice number please play it agin 4me. u know ma precious is away so it reflects much on me here.please diva.”
“Yo diva nakupongeza kwakufanya bonge la nyimbo iv ushawah kuimba au h ndo nyimbo yako ya kwanza?”ni cloud charles.
“Unajua nn diva!!?we ni mkali sana, umetisha ile mbaya yani mpaka daaah noumer,mtoto pale kati unavyolalamika Mmh,binafsi umenibamba.”
“Mimi hahahaha,kaaaliiii..ila ngoja,nimeiskiza kwy simu..subiri niingie hm,i need my Dre beats on...nivumilieni kidooogo nijiridhishe.” (MwanaFA)
Wengine nao hawakupenda kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, “Diamond umejishushia hadhi.mdada gani huyu umeimba naye? anaimba kama vile mjusi kabanwa na mlango, mashairi yenyewe kaiba ya Ray C!”
Mwisho, kamwe usidharau nguvu ya mitandao ya kijamii katika promotion ya muziki. Kwa uwezo wake wa kufanya promotion kwa mashabiki wake lukuki, wimbo huu utafika mbali na huenda ukampa hela kama alivyowahi kusema awali kuwa unaweza kutumika kwenye matangazo ya simu.
We might also change our minds and start dancing to the rhythm…….. Piga simu! Piga Simu! We out!
Sikiliza;
Monday, 11 June 2012
Ameen ya MwanaFA ni sample ya wimbo wa Cecile-Hey
Linapokuja
suala la kusample wimbo haijalishi kama msanii ni mkubwa ama mdogo watu
watasema na ukweli lazima utawekwa wazi. Kwa dunia hii ya leo yenye
maendeleo makubwa ya internet ukisample huwezi kujificha na hata
ukifanikiwa ipo siku wajanja watagundua tu.
Solothang ndiye aliyeligundua hili na sisi tukaamua kuhakikisha na kukuta kweli Ameen ya MwanaFA ni sample ya wimbo wa Cecile uitwao Hey aliomshirikisha Agent Sasco. Wimbo huu upo kwenye albam yake ya mwaka jana iitwayo Jamaicanization.
Producer wa wimbo huu ambaye ni Dully Sykes amesample wimbo huo kila kitu. Chorus yake mwenyewe Dully ni copy and paste ya chorus ya Cecile. Kipya kwenye Ameen iliyosifiwa sana wiki hii kwa maneno ya maana ya MwanaFA, ni mashairi tu.
Siku zote sampling pamoja na kuwa si jambo baya kihivyo huleta maana mbaya hasa kwa producer ambaye huonekana hana idea kiasi cha kuchukua za wengine.
Sikiliza mwenyewe na useme kama Dully Sykes ameonewa!
Mwaka huu pia Producer Samtimber wa Arusha alijikuta kwenye scandal hii baada ya kucopy na kupaste beat ya G-Unit kutengeneza ngoma ya Lord Eyes na Fid Q 'Neno'
Solothang ndiye aliyeligundua hili na sisi tukaamua kuhakikisha na kukuta kweli Ameen ya MwanaFA ni sample ya wimbo wa Cecile uitwao Hey aliomshirikisha Agent Sasco. Wimbo huu upo kwenye albam yake ya mwaka jana iitwayo Jamaicanization.
Producer wa wimbo huu ambaye ni Dully Sykes amesample wimbo huo kila kitu. Chorus yake mwenyewe Dully ni copy and paste ya chorus ya Cecile. Kipya kwenye Ameen iliyosifiwa sana wiki hii kwa maneno ya maana ya MwanaFA, ni mashairi tu.
Siku zote sampling pamoja na kuwa si jambo baya kihivyo huleta maana mbaya hasa kwa producer ambaye huonekana hana idea kiasi cha kuchukua za wengine.
Sikiliza mwenyewe na useme kama Dully Sykes ameonewa!
Mwaka huu pia Producer Samtimber wa Arusha alijikuta kwenye scandal hii baada ya kucopy na kupaste beat ya G-Unit kutengeneza ngoma ya Lord Eyes na Fid Q 'Neno'
Exclusive: Hermy B aeleza kilichotokea kati yake na AY
![]() |
Hermy B kulia akiwa na MC wa TPF |
Hermy B ambaye ameisoma makala hiyo, ametuandikia email kukanusha baadhi ya mambo tuliyoyaandika na pia kutoa ufafanuzi wa namna mambo yalivyokuwa na yalivyo sasa:
"Ningependa kujibu shutuma zilizoandikwa na blog yako kuhusu uhusiano wangu na swahiba wangu A.Y. Ningependa ifahamike kwamba mimi na A.Y kwa kipindi cha miaka 4 tumefanya kazi za muziki kwa karibu pamoja na kazi nyingine za biashara. Ni kawaida na inaeleweka kwamba mahali popote watu wanapofanya kazi pamoja kugongana katika mawazo au lugha ni jambo la kawaida, na ndio changamoto zenyewe. Si jambo la ajabu kama mimi na swahiba wangu A.Y. kupishana katika kazi.
Baada ya kusoma makala inayonihusu kwenye blog yako nimeona ni umuhimu wa kujibu ni makala yako haswa kuhusu swali linalohusu utu na tamaa ya pesa. Kwanza ningependa ieleweke kwamba umeniweka katika picha ya mtu mwenye tamaa kubwa ya pesa na nisiejali utu picha amabayo imeanza kunisumbua katika shuhuli zangu kwa muda mfupi tu kwani wananchi wameanza kuniona hivyo.
Hivyo nimeona ni lazima nijibu kwani nikiiacha bila kujibu madhara yake yatakuwa mabaya. Kwanza napenda uelewe sijawahi kuwa msimamizi wa kazi za A.Y zaidi ya kuwa producer wa nyimbo zake tu. Kipindi chote hicho nimekua natumia utaalamu wangu kwenye kutengeneza tu muziki wake. Maswala mengine yoooote amekuwa akifanya mwenyewe tena bila msaidizi.
Pia ufahamu bila A.Y na MwanaFA kunipa nafasi kutengeneza muziki wao nisingekua hapa nilipo. Nadhani inaeleweka mahali popote duniani kwamba kipaji ili kifahamike kwa watu lazima kipitie kwa mtu fulani au mkondo fulani. Si ajabu kama kipaji changu cha kuproduce muziki kimeweza kufahamika kwa kupitia kwa A.Y. Mimi sio mungu labda ningekua sehemu nyingine na mafanikio makubwa zaidi au machache zaidi,lakini nachojua rafiki yangu amenipa ngazi ya kufika huku nilipo sasa, sijawahi kuficha hilo na hata wao wenyewe wanajua na bado nashukuru kwa hilo.
A.Y hajawahi kuingia mkataba wa aina yoyote na kampuni ya BHits Music Group Limited wala mimi binafsi uliombana kufanya kazi na mimi na sio mtu mwingine yoyote. Nimetengeneza nyimbo zisizopungua 30 za A.Y, kwa ajili ya albamu yake katika kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2011. Baadhi ya nyimbo hizo zimeshatoka na nyingine bado zipo zikisubiri uhitaji wake. Wote tulikua na lengo la kutengeneza muziki kwa wingi na kuuza kwenye soko zuri la muziki ili tufaidike kwa pamoja.
Muda wote muziki ulikua unatolewa na unafanya vizuri kwa radio na T.V na show zilikua zinafanyika na zote nilikua nazijua iwe ndani ya nchi au nje ya nchi hii hata malipo nilikua nafahamu ni kiasi gani na sijawahi kufichwa na A.Y kuhusu hilo.
Utata umekuja kwenye malipo yaliyotajwa kwenye blog yako ambayo yameniudhi sana na baadhi ya wasanii wanaopenda kurekodi kwangu wameanza kuwasiliana na mimi kuuliza bei imepanda lini na kama inawahusu pia.
Kutoelewana kwetu kwetu kibiashara ilikuwa mwezi February mwaka huu yakihusu malipo ya album hiyo. Baada ya hapo niliamua kufunga mdomo wangu na nisingesema chochote kwani haya yalikua yananihusu mimi na rafiki yangu tu. Nimeamua kuongea sasa kwani nahisi nimeshambuliwa kwa mara ya pili kuhusu makubaliano haya na mara ya kwanza niliamua kukaa kimya.
Kwanza nataka ufahamu Katika kipindi cha kutokea 2008 mpaka leo hii (miaka 4) kwa matumizi ya nyimbo hizo, ambazo amekwishafanyia show nje na ndani ya nchi na nyingine kumpatia nominations na tuzo tofauti, nilichowahi kulipwa hakitaweza kuzidi shilingi milioni tatu kwa malipo ya awamu tofauti kwa miaka minne.
Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa kawaida anaehangaika kutoka.
Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi, ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja niliomba nilipwe millioni 2.
Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na niliona biashara hii itavunja urafiki wetu.
Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya. Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo bado hazijamixiwa, ila ampatie producer mwingine amfanyie hiyo kazi.
Mpaka naona hii makala A.Y hajaja kuchukua hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi.
Swala la mimi kuwa na wivu na kinyongo na mafanikio ya A.Y ni uongo na nashangaa umetoa wapi maneno hayo. Kama kulipwa kidogo, huku nikiona A.Y anaingiza fedha nyingi kwa muziki tunaotengeneza pamoja basi ningekua nimegombana nae toka mwaka 2009 labda.
Narudia kwamba nilikua najua kila show yake inapofanywa na sikuwahi kujisikia vibaya. Nataka utambue pia nilikua na akili timamu wakati nafanya kazi na A.Y na muda wowote nilikua na uwezo wa kubadili mawazo na kutaka tuandike makubaliano kwa karatasi ila sikufanya hivyo na wala sijutii chochote kwa utaratibu wetu wa hatari wa kufanya kazi bila mkataba wa maandishi na ndio maana nipo radhi hata sasa kumpatia nyimbo hizo bure kama nlivomwambia hapo mwanzo.
![]() |
AY |
Picha nyingine mbaya ulioichora ni kujaribu kuonyesha kuna kutopendana kati ya maproducer. Mimi Master Jay na Marco Chali ni marafiki wazuri tu na mpaka leo hii nikiwa na shida na nikamhitaji Marco Chali au Master Jay nitampigia simu bila aibu kwani hakuna ugomvi kati yetu. A.Y, Master Jay na Marco Chali pia ni marafiki wa siku nyingi na katika kipindi cha miaka minne akiwa Bhits kwa hiari yake na sio mkataba, A.Y amekuwa akienda MJ records anapojiskia na mara kadhaa mimi nimeenda na A.Y na mara kadhaa nimeenda peke yangu tena kwa ajili ya shughuli zangu binafsi.
Pia ufahamu katika kipindi hicho A.Y alikua akitumia muda mwingi MJ Records kuliko Bhits na hiyo yote ilikua ni mipango yake binafsi. A.Y hajawahi kuzuiwa kufanya kazi na mtu mwingine kwani ni msanii huru.
Ndugu yangu mimi ni mtu mpole nisiye na ugomvi na mtu hapa mjini. Nasikitika sana kwa jinsi kwenye makala yako ulivyojitahidi kuonyesha kwamba mimi na swahiba wangu tumejenga uadui.
Wasalaam
Hermes Bariki Joachim (Hermy B)
Managing Director"
Sunday, 10 June 2012
FlowTheBanks na Cyrill (Wakacha) waja na video ya Usiku na Mchana
![]() |
Wakacha |
Mara nyingi tumemzoea
Cyrill kwenye nyimbo za tambo, swagga na mapenzi lakini sasa anakuja na upande
mwingine ambapo atazungumzia maisha na pilika pilika za kila siku za kuukwepa
umaskini.
Hata hivyo atakuwa anampa
shavu tu member mwenzake wa kundi la Wakacha aitwaye FlowTheBanks aka GiggaFlow.
Kwa mujibu wa picha tuliyoipata
Facebook, Cyril anaonekana akiwa amevaa nguo chafu na ndala za njano zilizochoka.
Unaweza kumsahau Kamikaze!
![]() |
Cyril akiwa kwenye video set |
Kwenye picha hiyo kumeandikwa:
“@location,live on de set of ma homie flow frm WAKACHA,nyimbo inaitwa ucku na
mchana az a nu song of him,chorus km kawiz kapta ma homie kamikaze..pic by abba.”
The Rock aanza kujifua kwa Fast and Furious 6
Maandalizi ya toleo la 6 la
mfuliliizo wa filamu ya The Fast and the Furious yameanza rasmi.
Leo Dwayne Johnson aka The
Rock ambaye anaigiza kama polisi kwenye filamu hiyo amepost picha akiwa mazoezini na
kuandika;
‘Training for FAST 6
officially starts today..
You can run, but you can
never hide.. Ever.
Be sure to give your soul
to Jesus, cause your ass is mine.’
Saturday, 9 June 2012
Don Jazzy atweet namba za vocha kibao, usharp wako tu
Katika kuhakikisha kuwa jina lake na la label yake mpya ya Mavin Records inakuwa karibu zaidi na mashabiki, jana producer Don Jazzy ameamua kugawa voucher kibao.
Producer huyo ambaye jina lake ni Michael Collins ametweet namba za vocha za mitandao yote ya simu nchini Nigeria.
Kwa haraka haraka ametoa vocha zinazoweza kufikia thamani ya shilingi laki mbili hivi.
Anachofanya ni kuzitweet namba hizo na yule ambaye ataziona haraka na kuziingiza kwenye simu yake basi ndo atakuwa amepata vocha kirahisi hivyo.
“Thank you very much My great Don & Nigeria's № 1 producer for the voucher, I'm dancing *Azonto* #1500 unit No Joke o.” ametweet mmoja wa mashabiki walioziwahi credits hizo za bure.
Katika hatua nyingine jana Don Jazzy ameonesha kuwa licha ya kuvunjika kwa label yake na ‘D’Banj, Mo’Hits, bado wana mawasiliano mazuri kwa kumpongeza kwa kuzaliwa leo, “SHOUT OUT TO THE GREATEST ENTERTAINER OUT OF AFRICA @IAMDBANJ HAPPY BIRTHDAY BRO. HAVE ALL THE FUN IN THE WORLD. GOD BLESS.”
Wanamuziki walaani Manny Pacquiao kunyimwa ushindi dhidi ya Tim Bladley
Kama ulikuwa hujui ni
mchezo gani unaopendwa duniani baada ya soka leo jibu utalipata.
Boxing inapendwa jamani!
Alfajiri hii nchini Marekani kulikuwa na pambano la ngumi kati ya Manny Pacquiao
wa Ufilipino na Tim Bladley wa Marekani.
Bladley amepewa ushindi wa
pointi.
Pacquiao, ambaye mwaka huu
umaarufu wake uligeuka kama dini yenye wafuasi wengi ameshinda mapambano saba
mfululizo na imeonekana wazi kuwa ametawala pambano la leo, lakini ameshindwa.
Ndio maana wapenzi wa ngumi
duniani wamechukizwa sana na uamuzi huo wa wazi wa kumbeba Bladley. Wengine
wanahisi uamuzi huo umepangwa makusudi kwa maslahi ya biashara ili mabondia hao
warudiane mwezi November.
Hebu soma tweets hizi uone
jinsi Manny anavyoendwa na rapper/wanamuziki na watu maarufu.
Justin Timberlake
@jtimberlake
I'm gonna let it go...
After I say this... Boxing was RUINED tonight for me.
Expand
Amir Khan @AmirKingKhan
If Bradley wants it I'm
ready, he turned me down twice. After I beat Garcia I will offer Bradley the
fight for the 3rd time.
Kevin Hart @KevinHart4real
This is a setup.....this is
just a ploy!!!! This is The sport of boxing making Pacqaio & Mayweather
fight!!!! Look between the lines people
Drizzy @Drake
What an embarrassing night
for Boxing. Shit looked like the WWF. Pac Man and Jinky deserved to go home
happy.
SHAQ @SHAQ
I watched allota fights but
that decision was some bs. Now I wanna see pacqiou verses may weather I spelled
PAC mans name wrong so what lol
Rico Love @IamRicoLove
Wow!!! I guess Floyd can
retire now. #TTLO
Tank @TheRealTank
I'm always happy for my
black people but that decision was..... Only thing real about boxing is
@FloydMayweather #truth
Justin Timberlake
@jtimberlake
I cannot believe what I
just saw... Please tell me they read that decision wrong...
Trey Songz @TreySongz
Robbery!!!
Talib Kweli Greene
@TalibKweli
Bradley said he had to
check the tape. He should just check twitter actually.
RAEKWON @Raekwon
Worst Decision in boxing
I've have ever seen! Someone mustve got paid....
XZIBIT @xzibit
I live in LA, if I wanted
to see somebody get robbed,I could go outside and see it for free, it shouldn't
cost me 65 bucks. #PacBradley
Busta Rhymes @BusaBusss
BRADLEY U CAN'T SLEEP
2NIGHT THE FEEDBACK IS OVERWHELMING ISN'T IT? THE WORLD KNOWS U LOST. DO THE
RIGHT THING & GIVE THAT BELT 2 PACMAN!!!
KhloéKardashianOdom
@KhloeKardashian
So when Bradley checks the
tape.... And sees what we all saw... Will he give the belt to Pac? What winner
says they need to check the tape?
Producer wa ‘Niggas in Paris’ Hit-Boy aonesha uwezo wake wa kurap
Producer wa wimbo maarufu wa
Jay-Z na Kanye West – Niggas in Paris, Hit-Boy ameamua kuonesha kuwa yeye si
producer mkali tu bali ni bonge la rapper pia kwa kuachia ngoma iitwayo, "Jay-Z
Interview".
"Nilikuwa na jina
kabla hata sijauandika wimbo. Nilikuwa nalo kama miezi miwili iliyopita ama zaidi ya
hapo kama miezi minne hivi. Nilijua tu kuwa ni jina zuri la wimbo, niliuandika
kwenye notice zangu na kisha kupata beat kutoka kwa [producer] Bink.
Nilianza kuusambaza kwenye
mtandao na watu wakaupenda. MTV's Hip Hop POV waliuonesha kwenye TV na
ikanionesha nguvu ya mitandao ya kijamii (Vulture)
Pia producer huyo ameufananisha
wimbo huo na wimbo wa Kanye West, "Through the Wire” uliomtoa pia.
"I wanted to give
something personal and I would reference that video ["Through the
Wire"]. Just showing it ["Jay-Z Interview"] to people in the
last week or so, they automatically say that it reminds them of when they first
saw or heard Kanye, so I can't escape that."
Thursday, 7 June 2012
Sneakers za Kanye West zinauzwa TZS Mil.130 mtandaoni
Mashabiki wanaotegemea
kununua mapema pair ya viatu vya Kanye West viitwavyo Air Yeezy 2 Nike,
wanaweza kuanza kufikiria kuomba mkopo benki ili kumudu bei yake!
Mpaka sasa viatu hivyo
vinapigwa mnada kwa zaidi ya $90,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 130!.
Licha ya bei yake ya reja
reja kuwa ni $245 sawa na shilingi 377,300, dau la pair moja limepanda hadi
kufikia $100,000.
Uiagizaji wa kabla ya kuanza
kuuzwa rasmi kwa viatu hivyo (pre-order) umefikia hadi $90,100 kwenye mtandao
wa eBay.
Ingawa Kanye West, amekuwa
akivaa viatu hivyo kwa miezi sasa, uuzaji rasmi wa viatu hivyo vya Nike unaanza
kesho, June 9 na kuuzwa kwa $245. (ABC News)
Hata hivyo sneakers za Air
Yeezy 2 zitakuwa chache tu kwenye store shelves.
Nike inasema itatoa viatu
kuanzia pair 3,000-5,000. Japo kesho ndo vitaanza kuuzwa, mashabiki wameshaanza
kujipanga kwenye maduka kadhaa yatakayokuwa yanaviuza nchini marekani (Philly)
No comments:
Post a Comment