Ziara ya akina Misosi yapata pigo, Soggy aumia mguu kwenye mtumbwi
Wakati ziara ya wakongwe wa muziki wa Bongo Flava nchini,
Soggy, D-Knob na Bwana Misosi ikiwa haijamaliza hata wiki moja, imepata pigo
baada ya Soggy kuteleza kwenye mtumbwi kwenye visiwa vya Ziwa Victoria,
wilayani Sengerema, na kuumia.
Katika ajali hiyo Bwana Misosi tuliyeongea naye kwa simu
amesema begi moja limepotea.
Kwa sasa wao, yaani Misosi na D-Knob wapo wilayani
Sengerema, mkoani Mwanza, huku Soggy akiwa wilayani Muleba, Kagera kwa baba
yake.
“Baada ya kuanguka kwenye mtumbwi na kuumia mguu tumeamua
kusitisha show za visiwani kanda ya ziwa.Niko kwa Mzee Ngaiza-Muleba nakula
matoke tu,” ameandika Soggy.
Misosi na D-Knob waliobakia wilayani Sengerema wamesema
wamelazimika kusitisha show zao kwa siku sita na tayari wameshapiga show tatu.
Wameongeza kuwa kituo kinachofuata ni Mwanza mjini ambapo
Soggy ataungana nao huko kuendelea na ziara yao ya kanda ya ziwa.
No comments:
Post a Comment