Tuesday, July 10, 2012

Exclusive: Fid Q aongelea lengo la Hip Hop Darasa



Kila jumamosi,Fareed Kubanda huendesha darasa la hip hop la hiari jijini Dar es Salaam ambapo sasa limeanza kuwa maarufu. Leo tumeongea kwa simu na Fid Q kutaka kujua nini madhumuni ya darasa hilo na haya ni maelezo yake.

“Kwa haraka haraka hip hop darasa maudhui yake ni kuwafundisha vijana wawe na positive thinking na attitude kwa jamii, yaani wawe na fikira zilizopo katika mstari ulio sahihi na hata kitabia, kwahiyo tunawajenga hivyo kupitia muziki wa hiphop.

Hip hop darasa so far ina wanafunzi kama hamsini hivi na katika hao wanafunzi hamsini, arobaini ni watoto wa mtaani wote. Ninapoingia darasani mimi kama mwalimu,kuna vitu vingi sana najifunza. Kuna wengine wanakuja darasani hawajui kuandika lakini wanarap vizuri, kuna wengine wanakuja darasani hawajui kusoma lakini wanarap vizuri kwahiyo, tunafundishana mpaka kusoma na kuandika.

So far so good, tuna wanafunzi kama kumi wameimprove vizuri na baadaya mwezi mmoja naweza nikaanza kuwaonesha kwa watu kwamba hawa ndo wameimprove.

Mimi nafundisha somo la hip hop lakini kuna wawezeshaji wengine kama Churchil ambaye ni mtaalam wa masomo ya kujielewa na masuala ya leadership.”

No comments:

Post a Comment