Tuesday, July 10, 2012

SHOO YA DIAMOND YAVUNJA REKODI SONGEA

SHOO ya  nyota wa muziki wa kizazi kipya Bongo Naseeb Abdul 'Diamond' imeingia katka kitabu cha matukio yaliyokusanya watu wengi zaidi katika historia ya mji wa songea  na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Akizungumza na Teentz.com mapema leo Mkurugenzi wa Jambo Lee Club  ambayo iliratibu ziara nzima ya mwanamuziki huyo amesema kuwa shoo ya Diamond imevunja rekodi na kuingia kwenye kumbukumbu za watu  kwa kujaza watu wengi na pia  ikiwa ni shoo pekee iliyokuwa na msismko mkubwa  kuliko hata inavyokuwa  wakati wa michezo ya soka inayozihusisha timu kubwa na Simba na Yanga zinapokuja kucheza Songea.
"Shoo imefunika hakika haijawahi…

BOB JUNIOR ATUPIWA ZIGO LA LAWAMA

Mashabiki wa nyota wa muziki wa Kizazi kipya Bongo Junior wamemtupia zigo la lawama bosi huyo wa lebo ya sharobaro kwa kuwalaghai na kushindwa kutimiza ahadi kumwonyesha mke wake mtarajiwa wakati wa shoo yake aliyofanya ndani ya ukumbi wa Club Bilicannas jijini Dar.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Teentz.com mashabiki hao wlaiojitambulisha kuwa ni wakazi wa Gongo la Mboto walisema kuwa wameshindwa kumuelewa Bob Junior kwa kushindwa kuwaonyesha shemeji yao na kisha kukaa kimya bila kusema lolote tangu kufanyika kwa shoo hiyo jumapili iliyopita.
"Binafsi sikupendezwa na hali hile kwani licha ya kuja kuburudika, nia yangu kubwa ilikuwa ni kumuona mkewa wa Bob Junior msanii ambaye kwangu mimi ninamkubari kuliko wengine wote waliopo kwenye game" alisema mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kwa…

No comments:

Post a Comment