Leotainment's Picture of the day
![]() |
Kuanzia kushoto: Ney wa Mitego, Diamond, B12, Joe Makini na Fid Q tayari kwa show ya Wajanja ya Vodacom mjini Mtwara |
Nikki Mbishi amemdiss One The Incredible?
Okay, tunafahamu kuwa Nikki Mbishi na One The Incredible
ni watoto waliokuzwa na baba mmoja kimuziki (MLAB Studio) chini ya producer
Duke Touchez.
Mara nyingi wamekuwa wakifanya ngoma pamoja. Lakini kitu
kimoja tu ambacho Nikki hakifurahii kila asikiapo jina la One! Ni kwamba
wasanii wengi sasa hivi wanamuiga sana One katika uandishi na flow.
“EMCEES wengi wanataka kurap kama ONE The
Inkredibo,hawajui kuwa Maalim Nash a.ka.Nash Mcee pia ni mcee mwenye mitindo
hatari na hawajifunzi kupitia kwake#WAMEENEA KWENYE BOX NDO MAANA HAWAWEZI
KUFIKIRI NJE YA BOX#,” ameandika leo jumapili kupitia Facebook.
![]() |
Maalim Nash (kulia), mshikaji na Nikki Mbishi |
Kwanini tunauliza kama Nikki amemdiss One The Incredible?
Okay kama ulikuwa hujui ni kuwa kipindi Nikki Mbishi anatoka, alikuja na style
yake ya kipekee ya uandishi na mituo kwenye vina vyake. Kwa muda mfupi sana
style hiyo ikawaambukiza wasanii wengi wachanga. Kila mmoja akaanza kuandika na
kutua kwenye vina kama yeye.
![]() |
Nikki, Stereo, One na washkaji |
Kipindi hicho One alikuwa hajulikani kabisa. One amekuja
kujulikana kwenye ngoma waliyofanya yeye,
Nikki,Godzilla na kumshirikisha Belle 9 kwenye chorus,’Kila Siku’. Hapo
ndipo akagundulika msanii mwingine hatari kutoka MLAB!
One alipoachia debut single yake iliyoitwa The Incredible
ndipo wakampa salute zaidi na hata kutishia crown ya Nikki Mbishi. Hata hivyo
ukweli ni kwamba One aliwahi kukiri kuwa anamuogopa sana Nikki Mbishi kwa
uandishi!
Then tunapoona status kama hiyo iliyoandikwa na Nikki hasa
kwa kumsifia Nash mc dhidi ya One, it sounds like a potential diss to us! Let’s
wait.
Saturday, 7 July 2012
Nikki Mbishi kwa Fid Q – Nami sikuhitaji kama rafiki
Okay, tunajua ni utani tu lakini Nikki Mbishi aka Baba
Malcom ameandika hivi kwenye Facebook:
“Fareed Kubanda amesema "SIHITAJI MARAFIKI" kwa
hiyo mi nam-block leo rasmi na natangaza kuwa atabaki kuwa kaka angu wa hiyari
tu na si rafiki yangu teeeeeeena!!”
Kama ulikuwa hujui ni kwamba Fid ni miongoni mwa wasanii
wachache mno Tanzania wanaofanya hip hop ambao Mbishi anawakubali.
Uzuri ni kuwa hata Fid
pia anamkubali sana Nikki. Real recognize real! So it’s a mutual respect!
Leo, Juy 8, Fid atakuwepo Mtwara kwenye ‘Wajanja Tou’ ya
Vodacom.
No comments:
Post a Comment