HAWA NDIO WASANII WALIOSOMA NA KWENDA SHULE PAMOJA
Ommy
dimpoz mzee wa nai nai na baadae amesoma na super producer Mensen
Selkta akiwa amemtangulia kidato kimoko pale Mbezi High school
Mesen
Selekta yeye ni producer kutoka de fetality records lakini pia ni
msanii ambae keshatoa pini kama kushoto kulia, na nyamnyamu.
Jaffarai
amesoma na Jay moe kuanzia darasa la pili mpka la saba katika shule ya
msingi Makumbusho iliyoka kijitonyama Dar-es-salaam
Juma Mchopanga a.k.a Jay moe
Mangwea mzee wa freestyle amesoma shule moja na Mez B, Noorah na Daki Master katika secondary ya Mazengo iliyoka Dodoma
Mez B
Daki master
Noorah
Bob
jr ambae pini lake la Nichumu limekamata nafasi ya kwanza ndani ya
Top20 za Clouds wiki hii, amesoma na producer Nah Real ambae
ameshatengenez pini kama Pea ya Nikki wa pili na zinginezo katika shule
ya msingi Olympio.
Mzee
wa Ndehe mtini Feruz amesoma na jamaa wa Born Cruz waliowahi kutoa
ngoma iliyofanya vizuri iayoitwa kaka poa(wanamuita kaka poa huyu jamaa,
wanamuita mtoto wa watu huyu jamaa) katika shule ya sekondari ya
Makongo
Ben paul amesoma na Baghdadi Azania Secondary, lakini Ben Paul akiwa A level na Baghdadi akiwa A level
Baghdadi
Msanii
Suma Lee amesoma na Producer Duke kutoka M lab katiska shule ya
sekondari Sahare iliyoko Tanga huku Suma akiwa mbele ya Duke ki madarasa
Mh
Temba kutoka kiumeni amesoma shule na Solo Thang, Rich one, Chidi Benz,
Soggy Doggy, marehem Kanumba na Dazz baba katika shule ya sekondary ya
Jitegemee iliyoko Temeke, Dar es salaam
Sollo Thang
Chidi benz
Marehem Kanumba
: |
HIKI NDICHO ALICHOKIZUNGUMZA DIAMOND KUHUSU KUTO0KUELEWANA NA BABA YAKE MZAZI NA KAULI ALIYOITOA TID JUU YAKE
Baada
y amagazeti kuandika juu ya kutokuelewana kwa Diamond baba yake mzazi
pamoja na kauli aliyoitoa baba huyo kwa mwanae diamond amefunguka upande
wake pia. kwa sauti ya diamond mwenyewe akizungumza bonyeza hapa chini
Na hiki ndicho alichokizungumza kuhusu kauli ya TID pale alipomuita MPUMBAVU kwa kile kinachosemekana ANATUMIA jina la MNYAMA.
s: |
NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOFIKA KUMTEMBELEA KAJALA GEREZANI
Pichani
ni washkaji zake Kajala walioenda kumtembelea mida hii pale gereza la
Segerea na kuanzia kushoto ni Producer Lamar, Producer P.Funk Majani
mbele yake ni Shilole msanii wa Bongo Fleva na anayefuatia ni B12 kutoka
Clouds FM, VJ Penny, Sam Misago kutoka EATV na meneja wa Ommy Dimpozi
anaitwa Muba.
HATIMAE MTOTO WA KAMBO WA USHER RAYMOND AFARIKI DUNIA
Kyle Glover ambae ni mtoto wa mke
wa zamani wa Mwimbaji Usher Raymond, amefariki dunia leo kutokana na
kuumia kwenye ajali ya pikipiki za kwenye maji maarufu kama Jetski
mwanzoni mwa mwezi huu huko Georgia Marekani.
Madaktari
wametoa mashine zilizokua zinasaidia kumuweka hai mtoto huyo aliekua na
umri wa miaka 11 baada ya kugundua kwamba majeraha aliyoyapata
yasingeweza kutibika.
Kyle akiwa
na rafiki yake wa kike mwenye umri wa miaka 15 walipata ajali july 8
2012 huko Georgia baada ya Inner tube waliyokuwemo iliyokua ikivutwa na
boti kugongwa na Jetski wakiwa kwenye maji na hivyo kupata majeraha ya
kichwa.
MABESTE: KAA TAYARI KWA UZINDUZI WA WEBSITE YANGU
Leo
hii Mabeste amepiga story na mimi na kufunguka kuhusu mabeste website
pamoja na video ya "ALISEMA"..."Baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan,
nitaachia video yangu ya ALISEMA na pia nitaizindua website yangu
inayitwa http://www.mabeste.com/ , kwahiyo fans wangu watakuwa wakifaham vingi vinavyoendelea kuhusu mabeste kupitia website hiyo.." amesema mabeste...
ASANTE MWAJUMA KWA UPENDO WAKO KWANGU
: |
JANET JACKSON NA BILLIONEA BOO WAKE WAONEKANA WAKISPEND MONEY SARDINIA
Janet Jackson alionekana aki have fun na boo wake Wissam Al Mana akiwa Sardinia. Yup, ni pale pale alipoonekana Rihanna wiki hii.
: |
YANAYOJIRI KUNAKO
STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac
Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma
‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma.
Chanzo kilichopo mkoani humo,
kimepenyeza habari hiyo juzi, ambapo kilisema ukaribu wao uliamsha hisia
kwamba huenda wawili hao wamerudiana.
“Wapo wote huku Kigoma, kwa
Diamond ni sawa maana yupo na wasanii wenzake wa Kigoma All Stars, sasa
Wema amekujaje? Kwanza siyo mwanamuziki, lakini pia siyo mtu wa Kigoma
ni wa kutoka Tabora,” kilieleza chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hiyo, Ijumaa lilimvutia waya Diamond zaidi ya mara tatu lakini simu iliita bila kupokelewa.
Wema alipopigiwa simu alipatikana
na kufafanua ishu nzima ilivyo. Huyu hapa msikie: “Ni kweli nipo huku
Kigoma lakini sipo na Diamond. Nimekuja kwa mwaliko wa Zitto Kabwe
(Mbunge wa Kigoma Kaskazini).
“Mimi na Diamond ni marafiki tu,
hatuwezi kuwa wapenzi tena, kila mtu na maisha yake. Kifupi nina mtu
wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana.”
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake mpya alisema: “Kwa sasa siwezi kumtaja, lakini siku si nyingi nitamuweka hadharani watu wamjue.”
No comments:
Post a Comment