Sneakers za Kanye West zinauzwa TZS Mil.130 mtandaoni
Mashabiki wanaotegemea
kununua mapema pair ya viatu vya Kanye West viitwavyo Air Yeezy 2 Nike,
wanaweza kuanza kufikiria kuomba mkopo benki ili kumudu bei yake!
Mpaka sasa viatu hivyo
vinapigwa mnada kwa zaidi ya $90,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 130!.
Licha ya bei yake ya reja
reja kuwa ni $245 sawa na shilingi 377,300, dau la pair moja limepanda hadi
kufikia $100,000.
Uiagizaji wa kabla ya kuanza
kuuzwa rasmi kwa viatu hivyo (pre-order) umefikia hadi $90,100 kwenye mtandao
wa eBay.
Ingawa Kanye West, amekuwa
akivaa viatu hivyo kwa miezi sasa, uuzaji rasmi wa viatu hivyo vya Nike unaanza
kesho, June 9 na kuuzwa kwa $245. (ABC News)
Hata hivyo sneakers za Air
Yeezy 2 zitakuwa chache tu kwenye store shelves.
Nike inasema itatoa viatu
kuanzia pair 3,000-5,000. Japo kesho ndo vitaanza kuuzwa, mashabiki wameshaanza
kujipanga kwenye maduka kadhaa yatakayokuwa yanaviuza nchini marekani (Philly)
No comments:
Post a Comment