Tuesday, June 12, 2012

FlowTheBanks na Cyrill (Wakacha) waja na video ya Usiku na Mchana


Wakacha
Mara nyingi tumemzoea Cyrill kwenye nyimbo za tambo, swagga na mapenzi lakini sasa anakuja na upande mwingine ambapo atazungumzia maisha na pilika pilika za kila siku za kuukwepa umaskini.
Hata hivyo atakuwa anampa shavu tu member mwenzake wa kundi la Wakacha aitwaye FlowTheBanks aka GiggaFlow.
Kwa mujibu wa picha tuliyoipata Facebook, Cyril anaonekana akiwa amevaa nguo chafu na ndala za njano zilizochoka. Unaweza kumsahau Kamikaze!
Cyril akiwa kwenye video set
Kwenye picha hiyo kumeandikwa: “@location,live on de set of ma homie flow frm WAKACHA,nyimbo inaitwa ucku na mchana az a nu song of him,chorus km kawiz kapta ma homie kamikaze..

No comments:

Post a Comment