Exclusive: Hermy B aeleza kilichotokea kati yake na AY
![]() |
Hermy B kulia akiwa na MC wa TPF |
Hermy B ambaye ameisoma makala hiyo, ametuandikia email kukanusha baadhi ya mambo tuliyoyaandika na pia kutoa ufafanuzi wa namna mambo yalivyokuwa na yalivyo sasa:
"Ningependa kujibu shutuma zilizoandikwa na blog yako kuhusu uhusiano wangu na swahiba wangu A.Y. Ningependa ifahamike kwamba mimi na A.Y kwa kipindi cha miaka 4 tumefanya kazi za muziki kwa karibu pamoja na kazi nyingine za biashara. Ni kawaida na inaeleweka kwamba mahali popote watu wanapofanya kazi pamoja kugongana katika mawazo au lugha ni jambo la kawaida, na ndio changamoto zenyewe. Si jambo la ajabu kama mimi na swahiba wangu A.Y. kupishana katika kazi.
Baada ya kusoma makala inayonihusu kwenye blog yako nimeona ni umuhimu wa kujibu ni makala yako haswa kuhusu swali linalohusu utu na tamaa ya pesa. Kwanza ningependa ieleweke kwamba umeniweka katika picha ya mtu mwenye tamaa kubwa ya pesa na nisiejali utu picha amabayo imeanza kunisumbua katika shuhuli zangu kwa muda mfupi tu kwani wananchi wameanza kuniona hivyo.
Hivyo nimeona ni lazima nijibu kwani nikiiacha bila kujibu madhara yake yatakuwa mabaya. Kwanza napenda uelewe sijawahi kuwa msimamizi wa kazi za A.Y zaidi ya kuwa producer wa nyimbo zake tu. Kipindi chote hicho nimekua natumia utaalamu wangu kwenye kutengeneza tu muziki wake. Maswala mengine yoooote amekuwa akifanya mwenyewe tena bila msaidizi.
No comments:
Post a Comment