MESSI AVUNJA REKODI YA DUNIA!!
Mshambuliaji Lionel Messi alifunga mabao
manne na kutegeneza rekodi mpya yakufunga mabao 72 msimu huu na
kumwanga kocha wa Barcelona, Pep Guardiola kwa ushindi 4-0 dhidi ya
Espanyol ukiwa ni mchezo wao wa mwisho kucheza Camp Nou msimu huu.
Messi alifunga mabao hayo na kutoa
zawadi kwa kocha wake aliyemsaidia Margentina huyo kuwa mchezaji bora wa
dunia na Barcelona kuwa timu bora zaidi duniani.
Baada ya kufunga bao lake la 50 katika
La Liga msimu huu, Messi alikimbia na kumrukia Guardiola, ambaye
anaondoka baada ya kutwaa mataji 13 katika misimu nne.
Mchezaji mwingine aliyefunga mabao 70
katika msimu moja wa ligi daraja la kwanza ni Archie Stark akiwa na timu
ya Bethlehem Steel iliyokuwa ikishiriki Amerikani Soka Ligi (MSL)
ulikuwa ni msimu wa 1924-25.
No comments:
Post a Comment