Tundaman ataka Milioni 100 ili ajiunge na Watanashati
Jitihada za Ustaadh Juma wa Watanashati kumtaka Tundaman
awatose Tip Top Connection na ajiunge naye zimegonga mwamba.
Hiyo ni baada ya Tundaman kumwambia ili ajiunge na
Watanashati ni lazima aweke mezani dau la shilingi Milioni 100 cash!!!
Akiongea leo na East Africa Radio kwenye kipindi cha
Power Jams, Tunda amesema Ustaadh Juma ameshamtumia watu zaidi ya wanne
kumpelekea ujumbe wake uliokuwa ukimpa ofa ya shilingi milioni 10 ili ajiunge
na Dogo Janja, Suma Mnazaleti na wasanii wengine kwenye kambi yake ya watanashati.
Tunda amesema Ustaadhi huyo amepitia kwa watu wengi akiwemo
producer wake Manecky ili wamamshawishi ajiunge na watanashati.
Amedai kuwa kama kweli wana nia ya kumchukua
basi wampe dau hilo ili ahakikishe kuwa anagawa kiasi kwa Babu Tale, Abdul
Bonge wa Tip Top na familia yake ili aweze kuondoka kiroho safi.
Amesema akiondoka Tip Top ataacha pengo kubwa ambalo
haliwezi kuzibika kwa shilingi milioni kumi.
Tunda amekiambia kipindi cha Power Jams kuwa Watanashati
bado hawawezi kuleta impact yoyote nchini kutokana na wasanii waliopo na ndo maana
wanamhitaji.
Unahisi Tundaman ana thamani ya shilingi milioni 100?
Fid Q Rocks Vodacom Wanjaja Music Tour, Mtwara.
Hundreds of Wajanja
Music Tour fans in Mtwara were thrilled on Sunday evening by music star Farid Kubanda, popularly referred to as Fid
Q, forcing him to stay on stage even after his performance had ended.
The excited fans screamed and cheered Ngosha!Ngosha!Ngosha!as
Fid Q took to the stage a few minutes after fellow star, Diamond, finished his
show, and gave security guards a hard time to manage the fans
who later pushed his car in excitement not wanting him to leave.
Other artists who took the stage during the Mtwara music tour include
Shetaa,Joh Makini, Ney wa Mitego and Mabeste.
While addressing the media, Matina Nkurlu, Vodacom Tanzania
Public Relations Manager, said that the Wajanja Tour proceeds to Tanga this
coming Sunday, at Mkwakwani stadium.
“Wajanja tour is set for “waja leo waondoka leo” in Tanga.
The show really rocked Mtwara, so fans in Tanga better get ready for great
entertainment from various artists this Sunday,” said Nkurlu.
Video: The Game akimpa kichapo 40 Glocc(real video)
40 Glocc ni rapper kutoka California ambaye kwa muda mrefu
amekuwa akimtukana The Game kwenye YouTube na kujaribu kumharibia.
Sasa kwenye
video hii ni kama bahati tu Game akakutana na adui yake live kitaani (ndege tunduni) na kumpa kichapo
ambacho hakika hatokisahau katika maisha yake.
Video haipo clear sana lakini ukiiangalia yote utaelewa
kilichofanyika.
Imesambaa sana kwenye internet na 40 Glocc amesema hatofungua
mashtaka.
mashtaka.
New Music: Sheila Kwamboka (BBA 2008 na 2010) - Yours
Kwa wapenzi wa Big Brother jina la Sheila Kwamboka aka
Kwambox sio geni. Alianza kujulikana mwaka 2006 aliposhinda taji la Miss Tourism Kenya. Baada
ya hapo alifanya kazi kama ripota kwenye kituo cha runinga nchini humo mwaka 2008.
Mwaka huo huo akaiwakilisha Kenya kwenye Big Brother Africa na kisha kurejea
tena mwaka 2010 kwenye Big Brother Allstars.
Kwa sasa anafanya muziki, muigizaji na muongozaji wa filamu.
Video: Davido na Playback mwanzo mwisho, Stargame Eviction show
Jumapili iliyopita msanii chipukizi wa Nigeria, aliyejipatia umaarufu
ndani ya kipindi kifupi Davido, aliperform kwenye Eviction show ya Big Brother
Africa Stargame.
Ngoma aliyoperform inaitwa Dami Duro ambayo kwa sasa ni club
banger matata sana barani Africa. Ni ngoma kali to be honest!
Tatizo letu linakuja kwenye performance hii ambayo tunaweza
kuiita ya kitoto. Labda sisi tunasikia vibaya, lakini hata macho hayadanganyi
tukionacho kwamba kijana alikuwa akisynch mwanzo mwisho.
Tunafahamu kuwa show za
Big Brother hazisindikizwi na live band hivyo wasanii huimba kwa kutumia
beat chorus. Yaani msanii anaimba live kwenye
sehemu ya verse tu na zile back alizoweka studio ndo zinaweza kubaki
kwenye
beat kumsupport.
Lakini kwa show ya
Davido masikio hayatudanganyi kuwa tunachosikia mwanzo hadi mwisho wa
performance yake ni vocal tamu za studio na yeye akiruka
ruka tu na mpambe wake.
Tena tunahisi mic
zilikuwa zimezimwa kabisa sababu
hasikiki akiimba chochote! Hakuna haya yoyoyoyo! Damn! Why holding a mic
if you don't even sing!! Bahati yake ni kwamba ngoma ni kali, watu
wanaipenda
kwahiyo ilikuwa shangwe tu mjengoni na tena ukizingatia sound system ya
nguvu
iliyofungwa mle ndani, aahh ni raha tu.
Lakini mtindo huu unaoendekezwa na waandaji wa Big
Brother una hasara kubwa kwa wasanii wenyewe. Davido ni msanii mkubwa kufanya
performance kwa ‘kusynch’ (kujifanya unaimba wakati cd ya wimbo original
inaimba).
Huo ulikuwa ni muda kwake kudhihirisha kuwa si msanii wa studio tu
bali anaweza kufanya show kwa sauti yake halisi na watu bado wakaifurahia.
Pamoja na umaarufu wake, sisi tunasema hii ndio performance
mbaya kabisa tangu show hizo zianze kwenye shindano la Big Brother.
No comments:
Post a Comment