Justin Bieber anapenda kuwa na mama mwenye umri mdogo
Justin Bieber amesema kuwa karibu mno na mama yake kiumri,
ambaye alimzaa akiwa na miaka 18, kumewafanya wawe marafiki.
Mama yake na mwanamuziki huyo wa Canada anaitwa Pattie
Mallette.
Akiongea na 2Day FM, Justin amesema: "She's amazing...
Ni wazi nilikuwa kama ajali kwake, ni poa sana mama yangu bado ni mdogo, ni
rafiki na mama yangu pia, amekuwa strict sana siku zote, ameniweka kwenye
mstari.”
Katika mahojiano hayo Justin alizungumzia pia jinsi ambavyo
huwa haoni shida kuperform mbele ya maelfu ya watu lakini hupata shida kubwa
anapotaka kuongea mbele yao.
Alieleza:"Napenda kuperform, kupiga tour na kuwa na
umati mpya wa watu kila usiku, ni kitu nikipendacho siku zote.. Ni ajabu kuwa
naweza kuperform mbele ya watu wengi lakini ukifika wakati wa kuongea napata
shida, sijui kabisa jinsi ya kuzungumza mbele ya watu wengi."
Aidha Justin alizungumzia pia mipango ya kufanya filamu
ambapo amesema ameanza mazunguzo na muigizaji Mark Wahlberg kufanya filamu
mpya.
Nick Cannon: American Idol hawatamudu kumlipa Mariah Carey
Baada ya Jennifer Lopez na Steven Tyler kusema hawatorudi
tena kwenye msimu wa 12 wa mashindano ya
American Ido kama majaji, waandaji wake wanaendelea kuhaha kupata watu wa
kuziba mapengo yao.
Kuna taarifa kuwa Mariah Carey ni miongoni mwa masupastaa
wanaowataka waje waokoe jahazi.
Hata hivyo mume wake na Mariah, Nick Cannon amesema kama
watamtaka mkewe basi wajue kuwa yupo expensive kuliko wanavyoweza kufikiria.
“Sidhani kama wanaweza kumudu kumlipa Mariah Carey.
Anahitaji hela nyingi.
Kama walimpa JLo dola milioni 20, watatakiwa kulipa mara
mbili ya hiyo,” Nick aliuambia mtandao wa TMZ.
Tuesday, 17 July 2012
Sitaogopa ya Monica na Nisher yazidi kupenya
Wiki mbili zilizopita tuliandika makala kuupongeza wimbo wa
Monica na kaka yake Nisher wa Arusha kutokana na ubunifu wao wa kutengeneza
wimbo na video ya kisasa kwa muziki wa injili.
Wimbo huo upo kwenye mahadhi ya
rnb na video yake imetengenezwa kisasa tofauti na video nyingi za muziki wa injili
nchini ambazo huwa za kawaida sana.
Na sasa video hiyo imeingia rasmi kwenye top ten ya kituo cha runinga cha Channel 5 (EATV).
Kupitia Facebook, leo Nisher ameandika: CONGRATULATIONS to
Monica Davie Mona And Nisher Bybee For their FABULOUS MUSIC VIDEO!! The Video
Has Been Voted to AIR at The EATV's TOP TEN Charts TONIGHT!!! THANKKKSSSSS FOR
VOTING>>>> KEEP SUPPORTING NISHER's PROJECTS.
J.LO akanusha kuwa alitaka aongezewe dola milioni 2 kwa American Idol.
Jennifer Lopez amezikanusha ripoti kuwa alipigwa chini
na American Idol kwasababu alidai aongezewe malipo ya dola milioni 2.
Mwanamuziki huyo mrembo alitangaza wiki iliyopita kuwa
anaacha kuwa jaji wa shindano hilo siku chache baada ya jaji mwenzie Steve Tyler naye kusema anaipiga chini American
Idol.
Ingawa J-Lo alithibitisha kuhusu kujitoa kama jaji wa
American Idol kwenye interview na Ryan Seacrest kwamba ameamua kuondoka ili
kuendelea na mambo yake mwenyewe, alikubali pia kuwa asingeweza kuendelea bila
kuwepo Tyler.
"We had magic," Lopez aliiambia ABC News jumapili
iliyopita.
"I don’t know, with him gone, it might be a
different formula," nyota huyo aliongeza wakati akifanya concert yake ya Bell
Centre mjini Montreal.
Katika hatua nyingine, mume wa Mariah Carey, Nick Cannon
alizikanusha taarifa kuwa mke wake ataziba pengo la Jennifer kwenye show hiyo
na kudai kuwa Mariah ni expensive mno!!
Hata hivyo mwanamuziki mkongwe Aretha Franklin, mshindi
wa mara 18 wa tuzo za Grammy ambaye jarida la Rolling Stone lilimtaja kama ‘the
greatest female singer of all time’, wiki iliyopita alikiambia kituo cha
televisheni cha CNN kwa e-mail kuwa anapenda ajiunge na show hiyo kama jaji.
Franklin, 70, ni shabiki mkubwa wa show hiyo, na sasa
badala ya kuingalia kwenye runinga kama wamarekani wengine, yuko tayari
kuhusika katika kumchagua American Idol mpya.
Kuongezeka kwa Franklin kutasaidia kurudisha umaarufu wa
“Idol,” ambayo ilipoteza nafasi ya kama show bora ya mwaka kwa kuzidiwa na
kipindi cha NBC cha “Sunday Night Football.”
Kuwepo kwa mashindano mengine mapya ya aina hiyo
yakiwemo The X Factor na The Voice kumefanya American Idol pia kupoteza
watamazaji wengine.
Mtoto wa kufikia wa Usher bado hali ni mbaya
Mtoto wa kufikia wa Usher ambaye ni mtoto wa mke wake wa
zamani Tameka Foster, Kile Glover anasemekana kuwa bado ana hali mbaya tangu
apate ajali ya kugongwa na boti ziendazo kwa kasi wiki moja iliyopita.
Kile, alitangazwa kuwa ubongo wake umekufa siku chache tu
baada ya kukimbizwa hospitali baada ya kugongwa kichwani na boti hiyo.
Mtoto huyo mwenye miaka 11 amewekwa hai na mashine maalum
tangu ajali hiyo na vyanzo vimesema kuwa afya yake inazidi kuzorota.
Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa HollywoodLife kuwa muda
wowote anaweza kufariki kwakuwa hali yake ni mbaya.
“Lakini hakuna mtu anayemuambia kitu Tameka kwasababu hafikirii
kabisa kumuondelea mwanae mashine ya kumsaidia kuishi na bado anasubiria
miujiza,” kilisema chanzo hicho.
Wakati ambapo Usher amekuwa akitembelea hospitalini hapo na
kuwa pembeni ya kitanda alicholazwa Kile, watu walio karibu naye wamesema Usher
anahofia kumwambia Tameka kuwa akubali
tu hakuna la kumsaiidia mtoto wake.
Chege apata ajali mbaya ya gari
Msanii wa Kigoma All Stars Chege Chigunda usiku wa jana amepata
ajali mbaya ya gari maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zimesema kuwa usiku
huo Chege alikuwa ametokea jijini Nairobi.
Akiongea na mtangazaji wa Clouds FM, Diva kwenye kipindi
cha Ala za Roho, Chege amesema usiku huo wa saa nne akiwa kwenye gari alikutana
pikipiki katika mtaa mmoja wa maeneo ya Temeke ambaye alimgonga na yeye kupata
ajali hiyo.
Chege amepata majeraha kadhaa lakini anaendelea vizuri
licha ya gari lake kuharibika vibaya maeneo ya mbele.
![]() |
Hivi ndivyo gari la Chege lilivyokuwa baada ya ajali |
Haikuweza kufahamika mara moja hali ya mtu huyo aliyekuwa na
pikipiki.
Kupitia mahojiano hayo mafupi Chege amewatoa hofu mashabiki
wake kuwa hali yake ni nzuri na yupo salama.
Kupitia website yake,Diamond amempa pole mwanamuziki mwenzie
wa Kigoma All Stars kwa Nampa pole sana
msanii Chege Chigunda kwa Ajali mbaya ya gari,Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
yote yaliyotokea......
Tunafuatilia kwa karibu taarifa mpya zinazohusiana na ajali
hiyo.
No comments:
Post a Comment