Monday, July 30, 2012

Ben Pol alijua ‘Baadaye’ ya Ommy Dimpoz itakuja kuwa hit


Mara nyingi wasanii hupata fursa ya kusikiliza nyimbo za wenzao zinapokuwa kwenye hatua ya kutayarishwa.
 
Ben Pol aliusikia wimbo wa Ommy Dimpoz kabla hata ya kutoka na kumwambia kuwa utakuja kuwa tishio.
 
‘Unakumbuka niliwahi kukuambia kuhusu 'Baadae ,ona bro ,sasa nchi yote inaimba 'Baaadaeee eeeh'...hongeraaaa!!!,” ametweet Ben Pol kumwambia Ommy Dimpoz.
 
“Nakumbuka broo thanxxx,” alijibu Ommy.
 
Baadaye ni wimbo wa pili wa Ommy Dimpoz kufanya vizuri baada ya kuhit pia na wimbo wake wa kwanza, Nai Nai aliofanya na Ali Kiba.
 
Katika hatua nyingine Ben Pol amekuwa msanii wa kwanza Tanzania kuzungumzia habari ya msanii maarufu wa Marekani Frank Ocean kujitangaza kuwa ni shoga.
 
“Frank ocean anatuweka watu kwenye wakati mgumu ,ametoa album kali huku amejitangaza kuwa yeye ni gay ,kumuacha kumsikiliza nayo ni ishu,da!” amesema.
 
Hata hivyo hitmaker huyo wa ‘Nikikupata’ na mshindi wa tuzo za Kili, anaamini kuwa scandal hiyo haimpunguzii uwezo wake katika muziki.
 
“Haishushi ,ila bado wabongo sisi hatuwaelewi mashoga (mimi mbongo pia) ,ameni-dissapoint kidizain flani ,ila he's a gud singr/writer.”
 
Album ya Frank Ocean, Channel Orange ilikamata nafasi ya pili kwenye chart ya Billboard 200 na nafasi ya kwanza kwenye Billboard R&B/Hip-Hop Albums chart, kwa kuuza kopi 131,000 katika wiki ya kwanza.

Olimpiki: Kidunda 'adundwa' na Mmoldova

Picha: Jason Derulo akiperform nchini Rwanda

Rachel K wa Uganda kujaribu bahati American Idol ijayo

Keko asainishwa na Sony BMG Africa



Tuliliona hili linakuja mapema mno kutokana na uwezo wa rapper huyu. Hatimaye kweli imekuwa hivyo. Rapper wa kwanza wa kike nchini Uganda kupenya kwenye mainstream, Keko amekula mkataba na record label ya Sony BMG Africa.

Keko amekuwa akiwasiliana na Sony BMG Africa na amekuwa akifunga safari za hapa na pale kwenda Afrika Kusini kuzungumzia mchongo huo. Habari njema ni kuwa rapper huyo anayetamba sasa na ngoma ‘Make You Dance’ amechukuliwa rasmi.

Kwa sasa Keko anajiandaa kufanya collabo na msanii wa Afrika Kusini Toya Delazy ambaye naye yupo chini ya Sony.

Keko anaungana na mkenya Xtatic aliyesainishwa hivi karibuni na label hiyo pamoja na Rose Muhando ambaye alichukuliwa mwaka jana.

Sinta na Nyoshi El Sadaat kuja na ‘The Return of JLO'



Mwanadada Sinta na mwanamuziki wa kundi la Fm Academia, Nyoshi El Sadaat wanakuja na filamu iitwayo The Return of Jlo.
 
Filamu hiyo inayoongozwa na muongozaji maarufu wa kampuni ya Steps Entertainment, Selles Mapunda itaingia sokoni mwezi September, 2012.
Kupitia website yake, Sinta ameandika:
 
“Jumamosi saa nne na robo usiku ndio itakuwa habari ya mujini pale movie yangu ya the return of jlo itakapoanza vibweka vyake katika station yako ya star Tv.Ni vipande tuu,mpango mzima ni mwezi wa tisa, si ya kukosa ikiingia madukani maana I’m back like  never went. Saa ni saa nne na robo usiku.Star Tv  na Sauda mwana wa Mwilima.Glory be to God.
Sinta na Nyoshi wakiwa kwenye scene
Hata hivyo baadhi ya wasomaji wa website yake wameendelea kumkejeli kama ilivyo kawaida.
 
“Subiri tukusifie we mbwiga …..uzinduzi waufanyia hollyowood au kule kwenu kimara????? Kuchamba kwingi kushika mavi na usijidai baharia kumbe wajiharia, kuwa msomi kama unavyojinadi,” aliandika mmoja.
 
Selles Mapunda na Sintah
Mwingine alisema,”Dah kweli wewe u r not creative, bingwa wa kucopy paste sasa hivi atamwambia baby yake amnunulie nyumba iliaoneshe kwenye tv, kubwa jinga hili limama linaloshindana na watoto.”

(Video) Justin Bieber ft. Big Sean – As Long As You Love Me [Sneak Peek]

Friday, July 27, 2012

Picha: P-Unit na Collo ndani ya Juba, Sudan Kusini

Frasha ni mkare!
\

Tweets 11 za leo za Wema Sepetu zinazotia mashaka



Wema Sepetu si mtumiaji wa mara kwa mara wa mtandao wa Twitter. Huingia mara chache ndani ya wiki japo siku akiingia hutumia muda huo kuchat kidogo na washkaji na kuandika mambo yake mwenyewe. 

Lakini leo tangu tuanze kumfollow mrembo huyu, hatujawahi kuona akiandika tweets nyingi kiasi hiki kama leo na tena zenye ujumbe wa msichana mwenye maumivu moyoni! What’s wrong with her? What’s really going on? Hizi ni tweets kumi za Wema alizoziandika leo na kutupa mashaka!

1. Luv comes 2 those who still hope although they've bin disappointed, to those hu still bliv although they've bin betrayed, to those hu stil need to love although they've bin hurt b4 and to those hu hav da courage nd faith to build trust again...

2.Never say goodbye if u still want to try, never give up if u still feel u can go on, never say u don't love a person anymore if u can't let go...\

3.There ar things ud love to hear dat u wud never hear from da person ud like to hear dem from, but don't be so deaf as not hear it from da one hu says it from da heart...

4.Giving some1 all ur love is never an assurance dat they love u baq, don't xpect love in return, jus wait for it to grow in their heart, but if it doesn't, be content it grew in urz...

5.The best kind of friend is da kind u can jus be wit, never say a word nd then walk away feeling like it was da best conversation u have never had...

6.Wen the door of happiness closes, another opens but often times we look so long at the closed door dat we cannot see da one dat has bin opend for us..

7.A sad thing in life is wen u meet someone hu means a lot to u, only to find out in da end dat it was never meant to be and u jus hav to let go...

8.Love is wen u take away the feeling, the passion and the romance in a relation nd find out u still care for dat person..

9.Mayb god wants us to meet a few wrong people b4 meeting da right one so dat wen we finally meet da right person we will knw how to b grateful for dat gift..

10.It hurts 2 luv som1 nd nat b luvd in return, but wat is more painful is 2 luv som1 nd never find da courage to let dat person knw how u feel...

11.It is true dat u don't knw wat u got until u lose it but its also truee dat u don't knw wat uve bin missin until it arrives...

Seriously!! what the hell is going on? 

Hemed: Mabinti wa kibongo hawanivutii, nilishapita nao kama 32 hivi!



Tumekutana nayo hii kwenye blog ya mbunifu wa mavazi anayekuja kwa kasi nchini Martin Kadinda. Anasifika sana kwa kuwavisha mastaa wa Bongo zile suti za ‘marangirangi’ za single button, Hemed PHD akiwa mmoja wa ‘clients wake’.

So Martin alikuwa akipiga tu story na mteja wake na akamuuliza kama huwa anatumia condom kuwachapa nao! ‘We jamaa maswali gani hayo bana? mimi kondomu za nini? muda wote mimi nakwenda dry,” alijibu Hemed.

Kingine alisema kuwa jina lake la PHD limetokana na status yake ya kutembea na mademu kibao tena maarufu.

“Unauliza kengele kanisani??? unadhani kwanini naitwa Hemed PHD? nina taaluma ya kucheza na mioyo ya mabinti hawa wakibongo.... ila tatizo hawanivutii huwa napita tu kwakuwa nina hamu na wakati huo au ninakuwa sipo katika mahusiano na mtu yoyote,” alisema Hemed.


“Mpaka sasa nishawapitia 32... kwahiyo kuhusu majina katafute mwenyewe huko mtaani mbona stori zipo,” aliongeza.

Kwa kauli hiyo nadhani tumepata kirefu cha PHD,nacho ni PLAYER, HEARTBREAKER AND DESTROYER.

The Music Postmortem: Ngwair Ft. Mirror – Maskini Wenzangu


Wiki hii mwana Chamber Squad, Albert Mangwea ameachia ngoma yake mpya iitwayo 'Maskini Wenzangu' aliyomshirikisha Mirror. Producer wa ngoma hiyo ni Manecky wa AM RECORDS. Ijumaa ya leo panel ya TMP inauchana chana wimbo huo kuona mazuri na kasoro zake.

Josefly

Kama kawaida nitaegemea zaidi katika mashairi na utunzi kwa ujumla pamoja na jinsi ujumbe ulivyofikishwa kwa hadhira.
Kwa ufupi, Ngwair amefaulu katika utunzi, mpangilio wa matukio na mashairi. Idea kwa ujumla wake sio ngeni hasa ukizingatia kuwa kuna wasanii wengi tu wameshaimba kuhusu hali mbaya ya maisha ya watanzania na kilio kikubwa kikielekezwa kwa serikali. 
 
Lakini ubunifu alioutumia katika kuyaandika mashairi ya idea hii unaweza kuupa nafasi kubwa wimbo huu kueleweka vizuri na kuishinda ile hofu ya kwamba idea hii imezoeleka. Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi mtunzi alivyojitahidi kutumia sanaa ya ubunifu karibu kwenye kila mstari ambao ungeweza kuwa wa kawaida tu kama angeusema vile vile bila kutumia huu ubunifu. Mfano, ‘..Ndo maana wazanzibar wamechoka kutanga na nyika” hapo ujumbe kuhusu muungano..neno kutanga-na Nyika limetumiwa vizuri sana kuleta picha ya tatizo la muungano,…na maneno “big up Mandela leo South sio Africa” utaona neno South Africa lilivyotumika kusifia maendeleo ya South Africa.
 
Utunzi wa mtindo huu wa kucheza na maneno kama nilivyosema hapo juu unafanya verse ya kwanza kuwa fupi sana kwa kusikiliza. Pia mtunzi amefaulu kwa kiasi kikubwa kumfanya msikilizaji wa wimbo huu kuendelea kusikiliza zaidi kwa jinsi alivyoweza kupangilia na kumaliza na kitu kinachokuacha utafakari huku unasubiri ubeti wa pili… “leta mgomo baridi uijue serikali then muulize ULIMBOKA umuhimu wa madaktari. Hapa wengi watatafakari kwa sababu Ulimboka na swala la madaktari ni kitu ambacho kimeteka attention ya wengi Tanzania.
 
Hata katika ubeti wa pili na wa tatu ameendelea kucheza tu na maneno huku ujumbe ukiwa ni wa moja kwa moja (direct), mfano “tunaishi kiMungu-Mungu, toa M uweke Z upate kiZunguZungu”. 
 
Hapa msikilizaji pia atatafakari, na hapa atakua ameshirikishwa kuutafakari wimbo.akitoa M kwenye neno kiMunguMungu na akaweka Z.
Kila ubeti una maneno fUlani mazuri ya ubunifu tofauti na beti nyingine.

Naweza kusema kuWa huu mtindo alioutumia katika utunzi ndio umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana kufikisha ujumbe wa moja kwa moja na unaweza kuuongezea muda wa kuishi katika masikio ya wasikilizaji, ukizingatia matukio aliyoyaweka ambayo mengi ni ya hivi karibuni.
Tone aliyoitumia ni ya kulalamika ambayo inaendana kabisa na idea ya wimbo, ‘Nalia na masikini wenzangu’. Mdundo(beat) ni mzuri sana kwa jinsi ulivyofiti kwenye wimbo, kazi nzuri AM records.
 
Changamoto; kwenye ubeti wa tatu kuna maneno kama wanafanya maongezi hivi., yale maneno yanavutia sana kuyasikiliza lakini neno la kwanza halieleweki vizuri..anaongelea babu wa loliondo anasema “hivi babu wa loliondo……kwa siasa, hayo maneno ya katikati yanachanganya,sijui nguli, nduli au ni nini..Kumbe anasema "'hivi babu wa Loliondo nae inawezekana tu ilikuwa ni siasa)!(Lakini iko wapi hii kaburi ya Balali !?"...
Ila kwa ujumla kazi ni nzuri ,kwa mtazamo wangu.
 
Kinye
 
Mwezi huu baadhi ya wana hiphop wamegusa mambo muhimu sana yanayotugusa moja kwa moja kwa namna tofauti…tazama Fid Q  alivyogusia issue nyeti ya mahusiano, Chidi Benzino naye akajivisha ubaya ufanywao na kila mtu na kuuwasilisha kwa hadhira, Msafiri Kondo naye akaamua kuianika nchi kwa namna yake ya kipekee tofauti kidooogo na Albert Magwea aliyeamua kuchana waziwazi yanayojiri nchini kwa kuanika na kuhoji.
Binafsi nilimmiss Ngwair…siku zote nimekuwa nikimpenda yeye wa namna hii…nikimaanisha yeye wa kuimba nyimbo zilizo serious sana “ni kwasababu tu kuwa anaziweza sana”...kwa waliopata bahati ya kuisikiliza a.k.a mimi watakuwa wanaungana name kuguswa na nyimbo kama sikiliza, zawadi, na a.k.a mimi ukiicha pembeni Jah Kaya ambayo ilitugawa mashabiki wake “si sana”
 
“Masikini Wenzangu”…title nzuri ambayo inamshawishi kila mmoja kutamani kusikia kilichoimbwa ndani. Hakika kila kilichoibwa ndani kimenifanya nilibariki jina la wimbo huu na si kufanya ubatizo wa jina jipya.
Mwanzo wa wimbo “zile 8Barz” ulinipa ushawishi wa kuendelea kuusikiliza wimbo huu japo sekunde ya 31 ilinikereketa sikioni baada ya sauti ya Mirror kuingia ikiwa haiendani na Key ya beat ktk sekunde ile ambayo mpishi aliibadilisha beat kwa namna yake aijuaye “mimi si mtaalamu” lakini najua alifanya kitu kwenye beat.
 
“Mirror”…simjui huyu jamaa lakini anaonekana kama sio mgeni kwenye mic. Ana sauti nzuri na kiukweli amepata melody nzuri kwa chorus ya wimbo huu…shida yangu kwake kwenye uumbaji wa mdomo wakati wa kutamka maneno…niseme tu kuwa mpaka wakati naandika hivi sijafanikiwa kusikia nini anatamka kwenye maneno ya kwanza ya mzungunguko wa pili wa chorus “kabla ya tunasuffer”
 
“Maneke”…producer bora wa mwaka kwa mujibu wa zile tuzo…honestly speaking hii si production ya kusadifu title yako…hujafanya kitu tusahau alivyosound Ngwair kwenye production za Bongo Records, KamaKawa, na Tongwe!!! Japo hii ni miongoni mwa beat nzuri sana za Hiphop ulizowahi kunyonga!
 
Kiujumla wimbo ni mzuri na kwa kiasi fulani utamfanya Ngwair aendelee kuwa na heshima ya kuwa Nguli wa huu muziki wa Bongo.
J-Ryder
 
Ngoma ukiiskiliza first time, huwezi kataa ni nzuri..na ujumbe unaeleweka freshii tu.
 
Ila tuingie ndani zaidi na tuone vitu vinavyoweza kurekebishwa.
 
Upande wa instrument alizotumia, asilimia nyingi zina interfere na frequency za vocals..hasa wa chorus...male vocals mara nyingi frequencies zinakaa roughly between 200hz to 2500hz, so cutting some from the brass would be good, also ina depend unataka emphasis iende upande upi..so kama ziende kwa vocals, then u cut from brass na other instruments ambazo zina require.
Pitch bend effect whIch is also called tape stop effect, on 1st verse, inahitaji marekebisho pia. Timing/speed yake me naona haipo sawa..unless thats the result they wanted.
 
Zile Rhodes (instrument) kama unavyoiskia throughout the song, ina interfere na bass...pia inahitaji tu cut freqs on the rhodes..mfano anything below 40hz can be cut, so to allow space for the bass...na pia bass unaweza cut below 20hz ama 30 hz, because the human ear inasikia between 20hz to 20khz...anything below or higher is usually unheard.
 
Pia kwa chorus, vocals zina ''sibilance'' (A sibilant speech sound, such as English (s), (sh), (z), or (zh)....na hii sibilance ni pale unaposikia herufi, ama neno kwenye vocals kama ''s'' ''ch'' ''sh'' ambazo zinakuwa loud. Njia za kupunguza hii kitu, either kurekebisha pale vocals zinapokuwa recorded, ama kutumia de-esser plugin, multiband compressor, volume automation, zote hizi zinaweza saidia kupunguza ukali wa hii sibilance.

Sony Music presents: Troy Jamz with Kastenholt & Dee


The only RnB king of Scandinavia TROY JAMZ with KASTENHOLT & DEE are releasing a brand new hit single with SONY MUSIC. The song goes by the name of ''I'M IN LOVE''.
Troy Jamz is an international RNB artist, usic/video producer and song writer. The same guy who did the latest African HIT for an upcoming Tanzanian artists JanB and Obi ''Pretty Girl''. Troy Jamz is CLASSIC and his RnB album will be out soon this year. Listen I'M IN LOVE BELOW:

Updates:IGP wa Uganda aamrisha passport ya Chameleone irudishwe haraka

New Music: Bobby V Ft. Lil Wayne - Mirror


Video/Audio: Kumbe Chameolene ataperform kwenye Olimpiki,passport sasa!)





Chameleone aandamana kwenye ubalozi wa Tanzania Uganda kudai passport yake kwa Shigongo


Leo Jose Chameleone akiwa na mashabiki wake wanandamana kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kudai arudishiwe passport yake inayoshikiliwa na Erick Shigongo. Maandamano bado yanaendelea nje ya ubalozi huo jijini Kampala.
Jana kupitia facebook  aliandika mkasa mzima uliopelekea passport yake ishikiliwe. Huu hapa.
I AM VERY DISAPPOINTED!
Nilichukuliwa na kampuni ya GLOBAL PUBLISHERS, kampuni ya kitanzania kutumbuiza kwenye uwanja wa taifa Jule 7, 2012.
 
Nilitumbuiza kama mkataba ulivyokuwa. Jumapili ya tarehe 8, ERIC SHIGONGO ambaye ni mwenyekiti mtendaji wa GLOBAL PUBLISHERS aliichukua passport yangu kwa kumtuhumu meneja wangu kuwa amemtapeli dola 3500 ambazo kiukweli alitapeliwa na tapeli mmoja wa Kampala aitwaye George.
 
Nilisaidiwa na ubalozi wa Uganda mjini DAR EL SALAAM, ambao ulinipa passport ya muda kurudi nyumbani.
 
Niliporudi Kampala nilimtafuta tapeli huyo, nilimkamata na kumkabidhi kwa polisi ambao walimwachia katika makubaliano ambayo siyajui.
 
Nilieza haya kwa balozi wa Tanzania nchini Uganda kwa msaada lakini alinitosa.
 
Ni show zijazo Afrika Kusini, Uingereza, Ubelgiji, Norway, Sweden, Canada na kwingine. Hivyo ina maana Eric yupo juu ya sheria kukaa na passport yangu pasipo uhalali?
 
Mimi niumie kwa uzembe wake wa kumwamini tapeli?
 
Ni haki raia wa Tanzania asiye na mamlaka kushikilia passport yangu kwa zaidi ya mwezi? Nahitaji ushauri!
Aliendelea...
ERIC SHIGONGO AM BOUND TO MAKE YOU AN EAST AFRICAN CELEBRITY GOR TAKING THE LAW THE WAY YOU WANT! WE ARE PLANNING EAST AFRICA UNION AND U ARE PROMOTING YOUR SELFISH UNION! Damn

I AM AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION IN DEMOSTRATION FOR THE CONFISCATION OF MY PASSPORT BY A TANZANIAN ILLEGALY ERIC SHIGONGO I NEED MY FREEDOM TO TRAVEL AS A UGANDAN!
I NEED MY PASSPORT BACK ASAP!FOR GOD AND MY COUNTRY UGANDA.
 
Woken up! AM NOT GOING TO GO BACK TO MY HOUSE! AM GOING TO SLEEP AT THE TANZANIAN HIGH COMMISSION UGANDA UNTIL MY BROTHER FROM TANZANIA SURRENDERS BACK MY PASSPORT TO UGANDA GOVERNMENT THAT OWNS IT.HE IS HOLDING IT ILLEGALLY- IF NO BODY IS THERE FOR MY RIGHT AND JUSTICE LET ME ASK FOR IT MYSELF!
I AM DEMONSTRATING AGAINST INJUSTICE
AND WANT ERIC SHIGONGO TO RESPECT MY COUNTRY!
FOR GOD AND MY COUNRTY I DECLARE.



Godzilla auponda mfumo wa elimu Tanzania



Rapper mwenye swagga za 50 Cent, Godzilla ameukosoa mfumo wa elimu uliopo nchini ambao anadai hautengenezi wataalam. Kupitia mtandao wa Facebook, Godzilla ameandika:

Mfumo wa Elimu Tanzania inabidi ubadilishwe. Elimu ndefu sana na haiko katika kutengeneza wataalam(Experts).

Mfano mtu kasoma hadi darasa la 7 akafeli na mtu aliyesoma hadi Form6 akafeli wote wanakuwa sawa coz hawaajiliwi #so miaka yote imepotea bure.

Zamani kulikuwa hadi na la 4 la mkoloni wazee wakifika la 4 wanamaliza sa hivi aje wazee?!

Fanyeni mfumo mzuri wa Elimu ili tuwe na wasomi wengi.

Mawazo mazuri Godzilla.

Ushahidi:Diamond si 'mpweke' tena!

Facebook bana raha sana! Haifichi mambo! Ukibadilisha status tu washkaji wanajua! So kumbe Diamond alikuwa mpweke muda wote huo? Kwani yeye na Jokate waliishia wapi?


Tunafahamu wametosana kwa mujibu wa magazeti ya udaku na sio muda mrefu. Lakini kwa picha hiyo hapo juu inaonekana kama kijana alikuwa mpweke kwa muda sasa. Hongera lakini kwa kubadilisha status. Upweke haujawi kuwa mzuri. Ain't no fun when you are lonely!