Dogo Janja kufukuzwa Tip Top ni kumsaidia, kumrekebisha ama kumpoteza?
So kwa mujibu wa Teentz.com Dogo Janja amepigwa chini na TipTop! Kwetu
sisi halijatushangaza sana sababu tulijua ipo siku kama hii itafika. Ni rahisi
mno kujua tabia yake kutokana na kile anachokisema kwenye nyimbo zake. Ni dogo
fulani ukisikiliza mashairi yake utagundua tu kuwa ana usela usioendana na umri
wake.
Inasikitisha kwamba TipTop walimtoa Arusha na kumleta Dar ili wamtoe
kimuziki huku akiendelea na masomo yake kwa ridhaa ya wazazi wake, lakini
kufika huku na kufanya track mbili tatu dogo akajiona tayari ameshakuwa
supastaa!
Kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’ amesema kuwa Dogo Janja
ameshindwa kuendana na makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa
kundi hilo ikiwemo kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila
siku badala yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo
ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.(Teentz)
Uongozi wa Tip Top Connection unalijua game la Bongo na ndo maana
walimsisitiza kijana aishike elimu kwakuwa kuna
leo na kesho. Kwa umri wake mdogo kile kitendo cha kusikia ngoma zake
zinapigwa redioni, kitaa wanamkubali, madem wanashoboka, waandishi wa habari
wanampigia simu na kuomba appointment naye ya interview, kijana akajiona Bow
Wow!
“Katika hatua nyingine Madii amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na
kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi kufuatia
mafanikio ya muziki aliyoyapata akiwa na Tip Top Connection kwani hivi karibuni
alitega shule na kwenda kujificha nyumbani kwa TundaMan huku akimuaga Madii
kuwa anakwenda shule.”
Mtandao huo umeendelea kuandika, “kuona hivyo TundaMan aliamaua
kumuarifu Madii na mara moja kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda kumsaka,
lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa Madii anakuja aliamua kukimbia na
kwenda kujificha uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya
alikanyaga kuku na siri yake kujulikana kuwa amejificha hapao ndipo
alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho chake tayari kurejea ‘kileji’!!
Dogo Janja angejua jinsi kaka zake (baadhi ya wanamuziki wa Bongo
Fleva) waliocheza na kuidharau elimu na sasa wanajuta, asingeichezea bahati
hii. Tip Top walimpa fursa ya muhimu iliyomfanya hadi rais Jakaya Kikwete
amwalike kwenye Ikulu yake. Kama unakumbuka rais alimshauri kijana asome kwa
bidii na sio kutegemea tu muziki. Kumbe maneno hayo kutoka kwa mtu mwenye cheo
kikubwa zaidi nchini yalikuwa yanapita sikio la kulia na kutokea kushoto.
“Chezea madii ww! Safi sana
kiongoz kumrudisha ngarenaro akafanye usela nnya wake,DOGO PIMBI! Aliandika Donald
Mkulia.
Hata hivyo wengi wameuchukulia uamuzi huo kama si wa kujenga zaidi ya
kubomoa kama asemavyo huyu, “Maybe hili la kumtumia kwa maslahi yao binafsi
lina mantiki, yule si mtoto ambaye unaweza kusema harekebishiki, bado ni mdogo
na anarekebishika, hakuna ambaye hajaipitia hiyo hatua, fm 2 inaeleweka ni muda
wa foolish age mtoto kama yeye atapenda ajaribu kila kitu anachokiona. Wewe
kama mzazi wajibu wako ulikuwa ni kumkanya na kumsisitizia kusoma lakini si
kumfukuza. Je wazazi wawafukuze watoto zao wanapotega shule? sio solution. Au
kwa kuwa si damu yako, nahisi angekuwa damu yako usingemfukuza, usingekubali
kushindwa but it's not ur blood.”(Hameesha Ali)
“Safi sana rais wa tiptop kwakusimamia maadili ya vijana but dawa ya
jino sikung'oa nikutibu na pia dawa ya deni nikulipa nasi kulikimbia hivyo
mlipaswa kumdispline for any kind of punishment but kumfukuza nikukimbia
deniI,” aliandika mpenzi mmoja wa muziki,” alisema Mbaruku Mhina.
Lakini ndo hivyo tayari uamuzi umechukuliwa arudi nyumbani ili kama ni
usela akaufanyie huko huko Arusha kama
wengine wanavyosema, “welcome Arachuger dogo uje tukupeleke chimbo ukaive
baadaye urudi bongo kukinukisha mwenyewe Madii kitu gani bhana? Kwanza hapendi
Hip hop, shule kama hupendi kuna chuo cha kitaa.”
Kama Tip Top wasingefanya hivyo basi ipo siku wangekuja kulaumiwa na
wazazi wake kwakuwa walipewa ruhusa ya kumpeleka Dar wakijua atakuwa chini ya
usimamizi mzuri.
Na pia kwa haraka haraka hatudhani kama hawakuwahi kutoa taarifa hizi
kwa wazazi wake. Huenda wazazi wameongea mpaka wamechoka lakini hakujirekebisha
na kuwaomba Tip Top wamrudishe tu kwao na ndo maana kaka yake alikuwepo Stendi
ya Ubungo kurudi naye Arusha.
Ashukuru Mungu kuwa jina lake linajulikana tayari japo tayari watu
wameshamuona mhuni, asiyependa shule na mjinga.
Unauchukuliaje uamuzi huo wa Tip Tip?
No comments:
Post a Comment