New Music: Navio ft Nonini, Chameleon & Uganda All Stars – Dream Remix
Video ya Leka Dutigite:Siku mbili tu lakini ina views 11,123 Youtube
Let’s be honest, video hii imevunja rekodi za ngoma za Bongo
kwenye Youtube! Ndani ya siku mbili tu tangu iwekwe tarehe 31 July, 2012 kwenye
mtandao huo tayari imeangaliwa zaidi
ya 11,232 and counting!
Amini usiamini kufikia namba hiyo ndani ya siku mbili sio rahisi
hata kidogo.
Acha tuchukue mfano uelewe nini tunachomaanisha. Video ya Ay ft.
Marco Chali – Party Zone iliwekwa tarehe 15 July, 2012, hadi leo ina views 15,613.
Video ya Sihitaji Marafiki ya Fid Q ft. Yvonne Mwale iliwekwa tarehe 2 July,
2012 na mpaka sasa ina views 9,463. Hiyo ni mifano tu inayokupa picha ya jinsi
gani video hiyo itakuwa imeangaliwa ikifikisha mwezi mmoja.
Kitu kingine kinachovutia kwenye video hii ni pale Diamond
anapoonekana akiwa amekaa karibu na dada yake pamoja na Wema Sepetu upande wake
wa kushoto. Ni rahisi kugundua jinsi connection iliyokuwepo kati ya wapenzi hao
wa zamani kiasi ambacho kinatoa jibu la wazi kuwa huenda ni kweli wamerudiana.
![]() |
Angalia jinsi Wema alivyoshika mikono ya Diamond |
Haya bi baadhi ya maoni kwenye video hiyo.
“I'm a real 100% Muha from Marumba, Kasulu, Kigoma but born
and rose in Dodoma, I real like the song, this is what we want. Kigoma is a
historical region but among of the region on which the economy is developing
very slowly. " Abhantu bhakunda bhikongwa" but why we are poor?. Let
all of us promote our region by any means. I'm eager to know that water fall
location so that we can generate a micro if not a mini hydropower, Mr. Zitto or
anyone can you direct me where i can find it.”
“Wanna like this video like 1000 times, thou i wasn't raised
in KGM ila my blood has all elements of muha from manyovu, Kasulu. Nice song,
nice idea and by the way u guys have shown other artists that love and unity is
all we need. Ya'll keep doing what u gotta do to rep the mamaland KGM #Proud
Kigoma.”
EBSS kuanza kuruka jumapili hii kupitia ITV
Baada ya kuzunguka karibu mikoa yote kusaka vipaji vya
kuimba, jumapili hii ya August 5, show za usahili za Bongo Star Search, zitaanza
kurushwa kupitia ITV.
![]() |
Washiriki wa EBSS Dar wakipata maelekezo kadhaa mapema leo (August 2)
\ |
Usahili huo unamalizia kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa mwaka huu ataibuka na kitita cha shilingi milioni 50.
Leona Lewis sasa kurap, amwambia Minaj: 'I'm coming for you Nicki!'
LEONA Lewis ameamua kujaribu bahati yake kwenye rap na
albam yake mpya itakuwa imejaa michano tu.
Na mrembo huyo anajiamini kuwa atakuwa tishio kubwa kwa Nicki
Minaj ambaye hana mpinzani kwa sasa kibiashara.
Mwanamuziki huyo wa Uingereza kwa sasa anamalizia
malizia ngoma yake mpya ambayo anasema itakuwa tofauti kabisa.
Akiongea na gazeti la The Sun Leona amesema : "On
my new album I will be rapping. I've discovered my voice for rapping.
"I could probably go up against Nicki Minaj now.
I'm actually that good, so I'm coming for you Nicki! London style MCing."
Makala: Makosa yanayofanywa na wasanii wetu wakubwa
![]() |
Rama Dee |
Na Emmanuel Msigwa aka DJ Msigwa: Radio Journalist,
Presenter ,Radio DJ & Club DJ, Pride Fm Mtwara
Nimekuwa nikiumia sana kuona wasanii wetu ambao
tunawaita wasanii wakubwa, hapa nina imani unanielewa ninaposema “wasanii
wakubwa” na nikisema nitaje majina nahisi orodha itakuwa ndefu lakini leo
naomba nimtaje mmoja ambaye amekuwa sehemu ya wasanii ambao wanazikosea sana
kazi zao hasa video za nyimbo zao na nitaeleza wapi wanakosea,nini wanatakiwa
kufanya ili muziki wetu uweze kusonga mbele zaidi ya hapa ulipofikia.
Leo naomba nianze na RAMA DEE, huyu ki ukweli ni mmoja
kati ya wasanii wa Tanzania ambao mimi nawaona wana vipaji vya hali ya juu
katika aina ya muziki wanaoufanya hasa wanapofanya “rhythm and blues “ yaani
r&b nani ambaye hajui sauti nzuri ya jamaa huyu? Nani hajui ngoma kali
zilizofanywa na jamaa huyu? Na ni nani pia ambaye haujui ngoma kali alizoshiriki
kuzipamba kwa sauti yake tamu? Je unaikumbuka J.O.S.E.P.H ya Prof Jay?
Unaikumbuka ngoma kama RIDHIKA NAMI,
SARA,NAJUA na SIYO WAOAJI? Bila shaka hizi si ngoma ngeni masikioni
mwako…kifupi jamaa anaweza sana mimi ni mmoja kati ya mashabiki wake!
Kwa sasa jamaa ametoka na ngoma yake mpya inayoitwa KUWA
NA SUBIRA ambayo ndani wameshirikishwa rafiki
zake wa kitambo MAPACHA, umewahi kuisikia ngoma hiyo? Kama bado sikiliza
ngoma hiyo! Ngoma haina hata mwezi toka
ilipotoka yawezekana wiki mbili tu au tatu toka ilipoachiwa, nakumbuka mimi
nilikuwa mmoja kati ya watu waliandika katika “wall” zetu za facebook
niliusifia sana wimbo huo na kwangu mimi naona MAPACHA walistahili kuwepo
katika wimbo huo.
Licha ya uzuri wa wimbo huo bado napata mashaka ubora wa
wimbo huo unaweza kuwa wa muda mrefu? Je ngoma hiyo inaweza kukaa miaka hata
kumi (10) ukahit kama ilivyo sasa? La hasha!........sidhani! nakiri tena
sidhani! Kwanini? Unaikumbuka THRILLER
ya MICHAEL JACKSON? Unajua ngoma hiyo ilitolewa mwaka gani? Kwa taarifa yako ni
kwamba mtayarishaji wa muziki aitwaye
QUINCY JONES alitengeneza ngoma hiyo kupitia album iliyopewa jina hilo mwaka
1982 je ni miaka mingapi sasa? Je umewahi kuona video ya ngoma hiyo? Bila shaka
ndiyo!......sasa basi kama haufahamu ni kwamba ubora wa video hiyo ndiyo
uliifanya ngoma hiyo kung’ara mpaka sasa kwa nini wasanii wetu hawajifunzi
kupitia wao? Je awapati nafasi ya kujifunza kupitia ngoma fulani au ndiyo
kusema wanakurupuka?
Je umepata nafasi ya kuangalia video ya wimbo huo wa
RAMA DEE wa KUWA NA SUBIRA? Ni video nzuri kwa maana ya rangi,mandhari na
uchanganyaji wake wa picha! Vipi kuhusu
wahusika? Vipi kuhusu story board ya wimbo huo? Sijui gharama ya wimbo
huo lakini nina imani tena ya dhati kabisa kuwa video hiyo itaishusha sana
thamani ya ngoma hiyo kwa maana ya audio
yake, fumba macho wakati unaisikiliza ngoma hiyo halafu wakati huo huo tazama
video yake! Je kuna uhalisia wowote? Umewahi kuusikiliza wimbo wa SAME GAL wa
R.KELLY & USHER RAYMOND? Umewahi
kuona video yake?
Si huo tu ni nyimbo nyingi sana ambazo naweza kutolea mfano
ni kweli, RAMA DEE hajui hicho? Hakuna watu wa kuwashauri wasanii wetu? Au
wasanii wenyewe hawataki kuwashirikisha watu wenye upeo wa mambo hayo?
Inasikitisha sana! Ki ukweli ngoma nyingi kali za jamaa ambao ni audio
zinaangushwa na video zake si pekee yake bali wapo wengi nitawaelezea siku
nyingine!
Wakati fulani mwaka 2011 nilipata kushiriki katika mradi
mmoja wa waandishi wa habari nchini Ujerumani na kukaa huko kwa muda kuna kitu
kimoja upande wa sanaa nilichojifunza kule moja ya vitu hivyo ni namna
wanavyosimamia kazi za sanaa na pili ni namna kazi hizo zinavyotoka mathalani
album ya msanii au wimbo wa msanii utakaoucheza klabu za disko si ule
utakaousikisiliza redioni na kadhalika ni tofauti na utakaouona katika video na
wala hautafanana na ule wewe utakaoununua tofauti uanzia katika midundo “beats”
baadhi ya mistari “lyrics” wakati
mwingine hutofautiana katika melody zake, hivyo
ndivyo wenzetu wanavyofanya kikubwa zaidi ni kwamba nyimbo zao ubebwa na
ubora wa video zake na ndiyo maana wasanii wengi wa Marekani utoa kwanza video
za nyimbo zao kabla hajasambaza audio zao.
Tungependa kuona video za wasanii wetu zibebe pia theme
ya wimbo husika, kama mtu akizungumzia suala la kumsifia mpenzi/mke wake kwa
mapishi mazuri basi tuone kipande cha muhusika akipika na si kuona anachota
maji au kuona tabasamu lake!.............ndugu zangu, rafiki zangu wasanii
badilikeni hili kazi zenu zidumu miaka hata 30 zaidi ni kuboresha video za
NYIMBO ZENU!
Manecky azungumzia shutuma ya kuuza beat mara mbili
Producer wa AM Records, Manecky leo ameizungumzia kashfa
inayomkabili ya kuwagonganisha wasanii wawili wa hip hop aliowapa beat moja.
Wasanii hao ni Izzo B na mwingine aitwaye Brian huku
beat inayogombaniwa ikiwa ile ya wimbo wa Izzo B, ‘Mwaka Jana’.
Akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Manecky amekanusha kumuuzia
beat Briain kwa shilingi laki 3 kama msanii huyo alivyosema jana na kwamba
alimpa bure kwakuwa msanii huyo mara nyingi huenda kwenye studio hiyo na tayari
amesharekodi nyimbo kadhaa kwenye studio hiyo.
Akielezea namna beat hiyo ilivyotengenezwa Manecky amesema kuna siku alienda Maisha Club
ambako alikutana na wasanii kadhaa akiwemo Izzo na kuwasalimia. Anasema baada ya
kuwasalia kuna mtu mmoja maarufu ambaye hakumtaja jina alimskia akimdiss kuwa
yeye sio producer nali ni producer viduku.
Baada ya kuambiwa hivyo manecky ajisikia vibaya sana
kuamua kuondoka kwenye club hiyo.
"Nilimaindi kiukweli, cha kufanya sikurudi hata home , nikaenda studio, na beat nikagongea pale, ile siku nakumbuka nilifanya beat kama tatu, moja wapo ikiwa ile, ambayo the same beat, kama baada ya siku mbili tatu , tukawa tumeitwa kwenye vikao vya Kili Music vile, nikampa Izzo. Na that beat natengeneza moyoni mwangu. akilini mwangu nilikuwa natengeneza beat kwaajili ya Izzo B.
"Nilimaindi kiukweli, cha kufanya sikurudi hata home , nikaenda studio, na beat nikagongea pale, ile siku nakumbuka nilifanya beat kama tatu, moja wapo ikiwa ile, ambayo the same beat, kama baada ya siku mbili tatu , tukawa tumeitwa kwenye vikao vya Kili Music vile, nikampa Izzo. Na that beat natengeneza moyoni mwangu. akilini mwangu nilikuwa natengeneza beat kwaajili ya Izzo B.
Manecky anasema baadaye ndipo Brian alikuja kusikia ile
beat na yeye akaipenda na kuifanyia wimbo kwa maana kwamba baadaye producer huyo
angekuja kuweka vocal zake kwenye beat nyingine na tayari alikuwa amemwambia kuwa
ile ni beat ya izzo.
Eddo wa Ebony Fm azungumzia sababu ya kumpiga msanii wa Iringa
Jana tuliandika habari kuhusiana na msanii wa Hip hop wa
Iringa, Man Kichefu kudai kuwa amepigwa na mtangazaji wa Iringa Eddo Bashir. Leo tumezungumza
kwa urefu na mtangazaji huyo kuchukua yale yaliyopo kwa upande wake.
Eddo amesema kilichotokea anakifananisha na kitendo cha mdogo
kujaribu kumtukana mkubwa kwa makusudi ili kumuona mkubwa atafanyaje.
“Yule mtoto kimuziki mimi nimekua naye, mimi ofcourse
nilikuwa simjui lakini historicaly nimeambiwa kuwa kuna mtu mmoja anaitwa Meki
ambaye kamdissi pia kwenye hiyo track.”
Anasema Meki ndiye aliyempeleka Man Kichefu kwa
Amba (producer) ambaye alimfanyia wimbo bure iliyoitwa ‘Utanikumbuka’ ambapo
Amba aliimba chorus.
“Ile track imekuja mikononi mwangu, nikaiona nzuri
nikawa naipa airtime ya kutosha simjui na wala sijawahi kumtafuta,”anasema
Eddo.
Kutokana na kitendo hicho Eddo anasema Man Kichefu alifanya
jitihada za kumtafuta ili amshukuru kwa kumchezea ngoma yake hiyo.
“Mimi ndo mtu wa kwanza kumuita yule mtoto genious, na ana
nyimbo zaidi ya tatu na nimempa interview zaidi ya saba,namfeel kwasababu
anaweza kuandika.
Hakuna siku ambayo nimesema naomba kitu chochote kutoka
kwake pamoja na support niliyokuwa nampa, lakini kwenye nyimbo anaimba, mimi
naua muziki wa Iringa, mimi nachukua hela za wasanii kitu ambacho mimi nina watoto
ambao wananifuatilia ninachokifanya na wanacatch vile ambavyo vimeimbwa mule.
Mimi nahangaika na muziki wa Iringa karibu nakuwa chizi
na watu wanajua, hamna mtu ambaye hajapita kwenye mgongo wangu hata akifanya
interview asahau kunishukuru. Piga story na Mike, Mike anatoka kwenye mgongo wangu,
piga story na Squeezer, piga story na Dataz, piga story na Zay B,” Eddo
aliongeza.
Mtangazaji na DJ huyo anasema baada ya kutopendezwa na
kitendo cha Man Kichefu, aliamua kumuita studio ambapo hakukataa na kuanza kumkubusha
alikomtoa. Hata hivyo anasema msanii huyo aliendelea kuonesha dharau kwa
kumsukuma, kitendo kilichomuudhi.
“Kiukweli nilifanya kitu ambacho sikuwahi kukitegema
kukifanya, kwasababu pia mimi ni binadamu wa kawaida, nilikuwa na jaziba. Kweli
yule mtoto nimemchapa, sio kidogo, honestly na Mungu anisamehe, nimempiga sana
yule mtoto … sana.”
Eddo pia amemshangaa Man Kichefu kwa kitendo chake cha
kumdiss Amba kwenye wimbo huo wakati ni producer aliyemsaidia kwa mengi.
Hata hivyo amechukua nafasi hiyo kuwaomba radhi
mashabiki wake ambao hawajamwelewa kutokana na kitendo chake hicho cha kumpiga
Man Kichefu.
Sikiliza interview yote hapa:
Kwa upande wa shutuma zilizotolewa na msanii hiyo kuwa
Ebony Fm haitoi support kwa wasanii wa Iringa, mkurugenzi wa vipindi wa kituo
hicho cha radio hiyo, Renatus Kiluvia aka Bizzo amekanusha kwa kudai kuwa
hazina ukweli wowote.
Bizzo amesema Ebony Fm ina vipindi viwili vya muziki wa
Bongo Flava ambapo kimoja ni kwaajili ya nyimbo zote kwa ujumla na kingine
kikicheza nyimbo za wasanii wa eneo inaposikika redio hiyo katika mikoa ya Iringa,
Mbeya, Dodoma na Morogoro, Rukwa na Njombe.
![]() |
Bizzo |
New Music Video: Leka Dutigite - Kigoma All Stars
Diamond asumbuliwa na kifua alazwa kwa muda
Miezi ya hivi karibuni Diamond amefululiza kufanya show katika mikoa mbalimbali bila kupata mapumziko ya kutosha na huenda hiyo ndio ikawa ni sababu.
Kupitia Twitter Diamond ameandika "Dah hali yangu si nzuri, naumwaaa."
Tunamwombea Diamond apone haraka.
Breaking:Wasanii wapiga marufuku matumizi ya ringtone zao, wayapa makampuni ya simu siku saba
Umoja
wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rhumba, Dance, muziki wa Injili na aina
zingine leo umetoa agizo kwa makampuni yanayouza miito ya simu nchini
pamoja na makampuni ya simu kuiondoa miitio hiyo ndani ya siku saba
kuanzia leo
mpaka pale watakapokubaliana mikataba mipya.
Katika barua hiyo iliyoandikwa kwenda kwa waandishi wa
habari na iliyosainiwa na wasanii zaidi ya 150 nchini, wasanii hao wameyataka
makampuni ya simu kuondoa matangazo ya ringtone hizo kwenye radio, magazeti, tv,
website na kwenye ujumbe mfupi wa simu.
Hatua hiyo imechukuliwa na wasanii hao baada ya kubaini
kuwa makampuni ya simu yanawanyonya kwa kiasi kikubwa kwa kuwalipa chini ya
asilimia 10 ya mauzo ya ringtone hizo huku yenyewe yakibaki na zaidi ya asilimia
80.
Wiki iliyopita mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe aliliibua
suala hilo bungeni na kudai kuwa imeundwa kamati itakayoangalia upya utaratibu
wa mauzo ya ringtone.
Press Release ndio hii.
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA
BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya
muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio
kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na
Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta
mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo
tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja
na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya
kazi.
Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba
kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika
kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda
husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi
kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu,
jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja
ya pato toka kwenye shoo.
Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza
maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha
mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12
ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa
njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno
mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine
wanaendelea kusaini.
Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na
tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika
jambo hili.
Asante.
Exclusive: Mtangazaji wa Ebony FM Iringa ampiga msanii wa Hip Hop
![]() |
Man Kichefu |
Kupitia ukurasa wa Facebook msanii wa hip hop wa mkoani
Iringa Man Kichefu, leo ameandika, ‘jana nliitwa na eddo ebony.fm cha
kushangaza alinivamia na kuanza kunipiga akidai nimemchafua! Poa mi sina noma
ila nachoweza kusema its only the weak need to prove his strength through
force! My mom hits more than anyone I ever met!”
Kufuatia status hiyo tumempigia simu Man Kichefu ili
atueleze sababu ya yeye kupigwa na mtangazaji huyo.
“Kuna harakati fulani za muzki wa nyumbani hapa, unajue
eeh, jamaa (Ebony Fm) wanatudiss sisi wasanii wa hapa. Kwahiyo kitu kilichokuja
kufanyika kuna ngoma fulani sababu sisi kuna studio yetu tumefungua ,
tumejichanga tu mimi na mshikaji wangu tumefungua studio ,tumetengeza ngoma
moja kwahiyo hiyo ngoma tuliyoitengeza inaitwa ‘Himaya ya Mkwawa’ inaelezea
historia ya muziki wa Iringa na watu wa Iringa wale wanausuport muziki na wasio
usupport. Baada ya ngoma hiyo niliiyoifanya sababu nimeiweka tu kwenye internet
jamaa wakaichukua ile ngoma kitu kama wakaisikiliza hivi lakini mimi nikawa sijui.
Nikawa napewa tu taarifa kuwa jamaa anakutafuta kaongea
sana redioni. Mwisho wa siku juzi akanipigia simu mimi nikaipokea tu kwa roho
safi, ‘vipi bro, fresh fresh’ akaniambia
ebana na shida na wewe njoo ofisini.
Nikamwambia poa mimi nikaenda tu kwa roho safi. Ndio hivyo
yanii nimeenda ofisini jamaa akaniita akaanza kunitukana pale anadai nimemchafua,
kanivamia akaanza kunipiga.
Na baadhi ya wafanyakazi wengine yaani walikuja wakawa
wananishika wananiambai ebana twende huku tukaongee. Pale ofisini kwao kuna
sehemu moja nyuma ya ofisi kuna kibanda cha kupumzikia hivi, akaniita pale njoo
tuongee.
Nimefika hapo ndo akaanza kunishambulia sasa mimi nikaona hili eneo si
zuri sababu ni nyuma ya ofisi, nikakimbia nikaja nyuma ya ofisi.
Nimekuja mbele ya ofisi baadhi ya wafanyakazi wenzake
wakaja wakanishika bana twende huku wakawa wananirudisha tena kule ambako jamaa
alikuwa ananipiga yaani!
![]() |
Eddo mtangazaji wa Ebony Fm |
Kitu nilichokifanya mimi, nimefungua kesi polisi
kwasababu ya ulinzi wangu wa mbele au kitu chochote kitakachoenda kule mbele
lakini pia mimi sitaki nimfunge ama nimfanye lolote yaani.”
Tumemtafuta Eddo ili aeleze kwa upande wake lakini simu
yake haipatikani.
Sikiliza interview yote hapa
Sikiliza interview yote hapa
Huu ndio wimbo wa Man Kichefu ulioleta mgogoro.